Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini : Tupo tayari kukutana na Trump wakati wowote

Saa chache baada ya rais wa Marekani Donald Trump kujitoa katika mazungumzo yaliyopangwa kufanyika juni 12 huko Singapore na kiongozi wa Korea Kaskazini, Korea Kaskazini imeelezea kusikitishwa kwake na hatua hiyo.

Rais wa Marekani Donald Trump achukua uamuzi wa kufuta mkutano uliokua umepangwa kufanyika katika yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, Singapore.
Rais wa Marekani Donald Trump achukua uamuzi wa kufuta mkutano uliokua umepangwa kufanyika katika yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, Singapore. REUTERS/Kevin Lamarque and Korea Summit Press Pool/File Photos
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hizo pia zimeleta mshtuko kwa jumuiya ya kimataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ameelezea kuguswa na hatua hiyo ya Marekani. Naye rais wa Korea Kusini Moon Jae-In ametoa wito wa kuwepo kwa mkutano wa dharura wa viongozi wa juu wa usalama kuhusiana na suala hilo.

Trump amesema alikuwa 'akitazamia sana' kukutana na bwana Kim, huku akiongeza "kwa huzuni, na kutokana na hasira kubwa na uhasama wa wazi uliodhihirishwa katika taarifa yako ya hivi karibuni, ninaona kuwa sio sawa, kwa wakati huu kufanya mkutano uliopangwa kwa muda mrefu," Rais Trump alisema katika barua aliyomuandikia Kim.

“Hatua hiyo inarudisha nyuma jitihada kwa Korea kaskazini na ulimwengu, ” amesema Donald Trump huku akiongeza kuwa jeshi la Marekani liko tayari ikihitajikakujibu hatua yoyote isiyo na mpangilio kutoka kwa Korea kaskazini.

Kwa mujibu wa chanzo rasmi kutoka Korea Kaskazini, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un alikuwa amefanya jitihada zote katika maandalizi ya mkutano huo na kwamba Pyongyang ilikuwa tayari kuhakikisha tofauti zilizopo kati ya taifa lake na Marekani zinasuluhishwa kwa namna yoyote na popote.

Mkutano huu ungejadili namna ya uondoaji wa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea kufuatia mkutano wa Korea zote mbili uliofanyika mwezi April mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.