Pata taarifa kuu
UNSC-MYANMAR-USALAMA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili mgogoro nchini Myanmar

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana siku ya Alhamisi kujadilia hali ya kibinadamu nchini Myanmar. Maelfu ya watu kutoka jamii ya Rohingya wametoroka nchi hiyo na wengine wameuawa.

Meli ya wahamiaji wa rohingyas ikiwa katika baharini karibu na pwani ya Indonesia.
Meli ya wahamiaji wa rohingyas ikiwa katika baharini karibu na pwani ya Indonesia. AFP PHOTO / JANUAR
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress anatarajiwa kuwahotubia wanachama wa Baraza hilo na kuwaelezea hali ilivyo nchini humo baada ya wito wa kukomeshwa kwa mashambulizi dhidi ya watu wa jamii ya Rohigya.

Watau zaidi ua Laki mnne wamekimbilia nchi jirani ya Bangaldesha kwa kuhofia usalama wao.

Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteres alitoa wito kwa serikali ya Mynamar kuacha kutumia jeshi kuwalenga watu wa Jamii ya Rohingya.

Guteress ambaye, wiki jana alifungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani, aliitaka serikali kushughulikia malalamishi ya muda mrefu ya jamii hiyo.

Hivi karibuni kiongozi wa Mynamar Aung San Suu Kyi alisema yuko tayari kuwakaribsiha watalaam wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa kuja kuthathmini kilichosabisha jamii ya watu hao wa Kiislamu wapatao 421,000 kukimbia nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.