Pata taarifa kuu
MYANMAR-MAUAJI-USALAMA

Antonio Guterres aitaka Myanmar kuacha uhasama dhidi ya Warohingya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteres ametoa wito kwa serikali ya Mynamar kuacha kutumia jeshi kuwalenga watu wa Jamii ya Rohingya.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aonya dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya watu kutoka jamii ya Rohinya, Myanmar.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aonya dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya watu kutoka jamii ya Rohinya, Myanmar. DR
Matangazo ya kibiashara

Guteress ambaye amefungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani, ametaka pia serikali kushughulikia malalamishi ya muda mrefu ya jamii hiyo.

Kiongozi wa Mynamar Aung San Suu Kyi amesema yuko tayari kuwakaribsiha watalaam wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa kuja kuthathmini kilichosabisha jamii ya watu hao wa Kiislamu wapatao 421,000 kukimbia nchi hiyo.

Mkuu wa watalaam wa haki za Binadamu kutoka Umoja wa Mataifa inayochunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo Marzuki Darusman ametaka kuongezewa muda zaidi kuongezewa muda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.