Pata taarifa kuu
CHINA-USALAMA

Watu 41 wapoteza maisha kusini-mashariki mwa China

Maporomoko ya udongo yamewauwa watu 41 katika mkoa wa Fujian, kusini -mashariki mwa China, shirika la habari la Xinhua limearifu Jumapili hii likiwanukuu maafisa wa serikali.

Waokoaji wa China wakitafuta watu walionusurika baada yamaporomoko ya udungo yaliyovamia eneo la ujenzi katika mji wa Taining, kusini-mashariki mwa China, Mei 8, 2016.
Waokoaji wa China wakitafuta watu walionusurika baada yamaporomoko ya udungo yaliyovamia eneo la ujenzi katika mji wa Taining, kusini-mashariki mwa China, Mei 8, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Waokoaji 400 wa China wanaendelea na zoezi la wakitafuta watu walionusurika baada yamaporomoko ya udungo yaliyovamia eneo la ujenzi katika mji wa Taining, kusini-mashariki mwa China, Mei 8, 2016.

Kiwango cha matope cha mita 100,000 za ujazo pamoja na mawe vilishambulia usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili Mei 8, mitambo ya umeme ambayo bado inajengwa katika mji wa Taining, mkoani Fujian, shirtika la habari la serikali la Xinhua limebaini.

Mapema shirika hili la habari la Xinhua liliarifu kwamba watu 34 walitoweka baada ya maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha.

Watu saba wameijeruhiwa, shirika la habari la serikali limeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.