Pata taarifa kuu
BURMA-UCHAGUZI-SIASA

Burma: Aung San Suu Kyi atoa wito kwa viongozi wa Burma kwa mazungumzo

Kiongozi wa upinzani wa Burma, Aung San Suu Kyi, Jumatano hii, ametoa wito wa mazungumzo na viongozi wakuu watatu nchini Burma wakati ambapo matokeo ya awali ya uchaguzi wa Jumapili yanaonyesha ushindi wa kihistoria wa chama chake cha LND.

Taswira ya kiongozi wa upinzani wa Burma Aung San Suu Kyi ikionyeshwa kwenye makao makuu ya chama chake katika mji wa Rangoon, Novemba 9, 2015.
Taswira ya kiongozi wa upinzani wa Burma Aung San Suu Kyi ikionyeshwa kwenye makao makuu ya chama chake katika mji wa Rangoon, Novemba 9, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Upinzani umedai ushindi mkubwa katika uchaguzi wa wabunge wa Jumapili iliyopita. Tume ya uchaguzi imethibitisha kuwa chama cha LND cha kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi kimeshinda viti 211 kwa jumla ya viti 230. Chama cha majenerali wa zamani kilio madarakani kimekiri kushindwa na kuhakikisha kikotayari kukabidhi madaraka kwa amani.

"Wananchi wameonyesha nia yao katika uchaguzi", Suu Kyi ameandika katika barua aliowatumia mkuu wa majeshi Min Aung Hlaing, Rais Thein Sein na Spika wa bunge mwenye ushawishi mkubwa, Shwe Mann.

Aung San Suu Kyi amekiri kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili nchini humo haukuwa huru lakini ulikuwa wa haki, huku akiwapongeza watu wa Myanmar kwa kujitokeza kwa uwingi kushiriki uchaguzi huo.

Katika mkutano na waandishi wa habari hapo Jumanne wiki hii Suu Kyi amefahamisha kuwa chini ya katiba ya nchini hiyo hawezi akawa rais, lakini amesema yeye kama kiongozi wa chama atamteua rais.

Uchaguzi huo umechukuliwa na wengi kuwa ulio wa kidemokrasia zaidi katika miaka 25, baada ya miongo kadha ya uongozi wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.