Pata taarifa kuu
BURMA-UCHAGUZI-SIASA

Burma: ushiriki mkubwa katika uchaguzi huru wa kwanza katika miaka 25

Jumapili hii mamilioni ya raia wa Burma wameitikiwa kwa wingi na kwa utulivu uchaguzi huru wa kwanza nchini humo katika kipindi cha miaka 25, ambapo Aung San Suu Kyi amepewa nafasi kubwa ya ushindi, baada ya miaka ya kadhaa ya upinzani.

Aung San Suu Kyi, mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel, amepiga kura Jumapili asubuhi katika shule ya katikati ya Rangoon.
Aung San Suu Kyi, mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel, amepiga kura Jumapili asubuhi katika shule ya katikati ya Rangoon. EUTERS/Soe Zeya Tun
Matangazo ya kibiashara

Hakuna matokeo kamili ambayo yatatangazwa baada ya siku kadhaa katika nchi hiyo maskini kwa uongozi wa madhalimu, bila utamaduni wa uchaguzi.

Vituo vya kupigia kura vimefungwa kwa wakati, baadaye jioni, na tume ya uchaguzi imetangaza 80% ya ushiriki ya wapiga kura zaidi ya milioni 30, kulingana na makadirio ya awali. Matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa Jumatatu asubuhi.

" Subiri matokeo nyumbani kwako. Na wakati matokeo yatatangazwa, nataka muyakukubali kwa amani " , amesema Aung San Suu Kyi, ambaye raia wa Burma wanamwita kwa jina la utani "mama Suu". Aliyasema hayo katika ujumbe aliousoma nmbele ya umati wa watu waliokuja kumsikiliza, wakati wa usiku, mbele ya makao makuu ya chama chake.

" Nampenda Mama Suu, kwa upendo wa dhati .... ntabaki hapa mpaka matokeo yatangazwe ", ameema Tin Tin Oo, mwanaharakati wa miaka 44, miongoni mwa maelfu ya raia wa Burma waliokusanyika kusherehekea ushindi . Baadhi walitawanyika, wengine walikata tamaa kwamba Mama suui hakuja kujiunga na wengine katika sherehe.

Wakati huo huo Marekani imesema imefurahishwa na namna ambavyo uchaguzi huo ulivyofanyika.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema nchi yake ina matumaini makubwa kuona demokrasia inaimarishwa nchini humo.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema huenda uchaguzi huo ukaamua hatima ya kisiasa ya kiongozi wa chama kinachounga mkono demokrasia cha Aung San Suu Kyi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.