Pata taarifa kuu
URUSI-UKRAINE-Msaada

Msaada wa kibinadamu unaendelea kuzua mvutano kati ya Ukraine na Urusi

Msaada wa kibinadamu uliyotolea na Urusi kwa raia wa mashariki mwa Ukraine unaendelea kuzua mvutano kati ya Moscow na Kiev. Takribani magari 300 ya Urusi yamezuiliwa kwenye mpaka wa Urusi na Ukraine.

Msafara wa magari ya Urusi yakielekea Lugansk, mji unaoshikiliwa na waasi wa Ukraine.
Msafara wa magari ya Urusi yakielekea Lugansk, mji unaoshikiliwa na waasi wa Ukraine. REUTERS/Maxim Shemetov
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Ukraine wanaendelea kushuku kwamba huenda msaada huo wa kibinadamu ni kisingizio ili Urusi iingiliye kijeshi taifa la Ukraine, hususan kuwapa silaha waasi wanaopigana na jeshi la Ukraine.

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mabilimbali, ambao wanafuatilia msafara huo wa magari ya Urusi unao endelea kuwa karibu na mpaka wa Urusi na Ukraine (kusini), wamebaini kwamba magari ya kijeshi ya rangi ya kaki yamekua yakionekana karibu na msafara huo wa magari meupe yanayodaiwa kubeba msaada wa kibinadamu nchini Ukraine. Hata hivo helikopta ya jeshi pia imeonekana ikipaa juu ya msafara huo, hali ambayo imezidisha hofu kwa serikali ya Ukraine.

Imeonekana kuwa baadhi ya magari hayo yameingia katika mji wa wa Kamensk Shakhtinsky katika jimbo la Rostov, nchini Urusi, karibu kilomita zaidi ya thelathini na mpaka wa Ukraine, unaoshikiliwa kwa sehemu kumbwa na waasi wa Ukraine.

Msafara unaelekea Lugansk

Jumatano wiki hii, Kiev, imetoa masharti ili magari hayo yaweze kuingia nchini Ukraine, ikiwa ni pamoja na msaada huo kukabidhiwa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu na ICRC ili mashirika hayo yawafikishiye walengwa. Msafara huo ulioondoka tangu juzi katika jimbo la Moscow, ambao ungeliingia hadi katika mji wa Kharkiv, ulikua unasubiriwa kwenye mpaka ulioko kaskazini mwa Ukraine.

Lakini msafara huo umegeuza njia na kwa sasa umewasili kusini mwa jimbo la Rostov, jirani na jimbo la Lugansk mpakani mwa Ukraine, ambako itakua hatua ya mwisho ya msafara huo.

Serikali ya Ukraine imewataka askari polisi walioko mipakani kukagua na kupakua vyote viliyomo ndani ya magari hayo kabla hayajaingia nchini Ukraine, la sivyo, Kiev imetishia kuzuia msafara. Kinachobaki sasa ni kujua itakuaje, wakati eneo msafara huo unako elekea liko mikononi mwa waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.