Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-Msaada-Usalama

Magari ya Urusi yanayobeba msaada wa kibinadamu yanaelekea Ukraine

Msafara wa magari 280 ya urusi bado unaendelea  ukielekea kwenye mpaka wa Urusi na Ukraine. Magari hayo yaliondoka jumanne asubuhi wiki hii katika kambi ya jeshi la Urusi katika jimbo la Moscow, na yanasubiriwa jumatano jioni wiki hii katika jimbo la Belgorod.

Msafara wa magari ya Urusi yakielekea nchini Ukraine.
Msafara wa magari ya Urusi yakielekea nchini Ukraine. REUTERS/Nikita Paukov
Matangazo ya kibiashara

Upande wa Urusi, suala hilo limeshaeleweka. Taarifa zote kuhusu operesheni ya Urusi ya kuwatolea msaada raia wa Ukraine, imejadiliwa na serikali ya Ukraine, waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Serguei Lavrov, amethibitisha

“Tumetekeleza matakwa ya Ukraine, bila hata hivo kwenda kinyume nayo. Tumekubali kufuata utaratibu uliyopendekezwa na Ukraine, na sisi tumeona kuwa utaratibu huo ni mzuri. Tumekubaliana na serikali ya Ukraine namba zao za usajili wa magari ziwekwe kwenye magari yetu, wakati zitakua zimeingia nchini Ukraine”, amesema Lavrov.

Waziri hyo wa mambo ya nje wa Urusi, amebaini kwamba wamekubali pia kuwashirikisha wajumbe wa shirika la msalaba mwekundi na maafisa wa Jumuiya ya usalama na maendeleo ya Umoja wa Ulaya katika zoezi hilo la kuingiza msaada wa kibinadamu nchini Ukraine.

Jumanne wiki hii, ikulu ya Kiev ilieleza kwamba haitokubali magari hayo ya Urusi yaingiye nchini Ukraine, huku ikitoa masharti ya kukabidhi msaada huo shirika la msalaba mwekundu magari hayo yatakapowasili mpakani.

Kauli hiyo imemshangaza Serguei Lavrov : “ Tumepata taarifa inayothibitisha kwamba serikali ya Ukraine imekubali kupokea msaada huo. Nafikiri kwmba kauli hiyo ya mwanzo ya serikali ya Ukraine itakua haina tena nguvu, kwani suala hilo tumelijadili na serikali ya Ukraine".

Msimamo huo wa kuubali msaada kutoka Urusi umekua ni gumzo nchini Ukraine, ambapo Moscow imekua ikituhumiwa kwamba inasaidia kijeshi na kuwapa silaha waasi nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.