Pata taarifa kuu

Benin kutuma wanajeshi 2,000 nchini Haiti

Benin inashikilia mpango wake wa kushiriki katika Misheni ya Msaada wa Usalama wa Kimataifa nchini Haiti (MMSS). Maendeleo ya hivi punde ya kisiasa hayabadilishi chochote. Nchi hiyo itapeleka wanajeshi 2,000 kusaidia polisi wa Haiti kupambana na magenge yenye silaha nchini humo, kwa mujibu wa habari kutoka kwa mwanahabari wetu nchini Benin, Jean-Luc Aplogan.

Wanajeshi wa Kitengo cha Usalama Mkuu wa Ikulu ya Kitaifa, USGPN, walitenga eneo la usalama kuzunguka moja ya vituo vitatu vya polisi katikati mwa jiji baada ya polisi kuzima shambulio la genge lenye silaha siku moja kabla, huko Port-au- Prince, Haiti, Machi 9. , 2024.
Wanajeshi wa Kitengo cha Usalama Mkuu wa Ikulu ya Kitaifa, USGPN, walitenga eneo la usalama kuzunguka moja ya vituo vitatu vya polisi katikati mwa jiji baada ya polisi kuzima shambulio la genge lenye silaha siku moja kabla, huko Port-au- Prince, Haiti, Machi 9. , 2024. AP - Odelyn Joseph
Matangazo ya kibiashara

Mwanzoni mamlaka ilitaja idadi ya wnajeshi 1,500 ambao watatumwa nchini Hiati kusaidia polisi wa Haiti kukabiliana na magenge yenye sila na kurejesha utulivu. Wanajeshi hao wanatoka kwa vikosi vya anga, ardhini, baharini na kikosi cha walinzi wa taifa. Askari watakaoondoka tayari wamejulikana, bado wanakaguliwa kwa hatua ya mwisho, hakika uchunguzi mdogo kwa kila mmoja wao. Kisha watafunzwa na wakufunzi wa Benin na wa kigeni.

Vyanzo vingine vinabaini kwamba wanajeshi wa Benin wanaweza kuwa tayari kuondoka ndani ya miezi mitatu au minne. Matumaini kidogo sana kama ratiba, kulingana na wale waliozoea shughuli za aina hii. Ni lazima kuzingatia ufadhili na muda wa malipo ya awali ya fedha. Marekani na Canada ndizo wafadhili wakuu.

Mikutano itatangazwa katika wiki zijazo. Benin daima imekuwa ikichangia pamoja na polisi na askari wake katika misheni ya usalama nchini Haiti kutokana na mshikamano lakini pia kwa sababu ya uhusiano wa kihistoria na kitamaduni. Wengi pia wanaona faida ya kidiplomasia kwa Benin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.