Pata taarifa kuu

Jamhuri ya Dominika: Ishirini na moja wafariki baada ya mvua kubwa kunyesha

Mvua kubwa iliyonyesha nchini Jamhuri ya Dominika katika muda wa saa 48 zilizopita imesababisha vifo vya takriban watu 21 wakiwemo watoto 3, mamlaka imetangaza.

Gari la polisi likizunguka nguzo ya umeme iliyobomolewa na Kimbunga Irma mnamo Septemba 7, 2017, Nagua, Jamhuri ya Dominika.
Gari la polisi likizunguka nguzo ya umeme iliyobomolewa na Kimbunga Irma mnamo Septemba 7, 2017, Nagua, Jamhuri ya Dominika. REUTERS/Ricardo Rojas
Matangazo ya kibiashara

Watu wanne kati ya waliofariki katika matukio tofauti ni raia wa Marekani na watatu ni Wahaiti, kulingana na Kituo cha Operesheni za Dharura (COE). Takriban majimbo yote nchini (30 kati ya 32) yalikuwa katka hali ya wasiwasi siku ya Jumapili, kulingana na mamlaka.

Vifo tisa kati ya 21 vilitokea Jumamosi jioni wakati ukuta mkubwa ulipoangukia magari kwenye mtaa wa Februar, mojawapo ya maeneo makuu ya Santo Domingo. "Tukio hili liligharimu maisha ya watu tisa," ilisema Wizara ya Ujenzi wa Umma katika taarifa kwa vyombo vya habari ikisisitiza kwamba "uchunguzi" ulifunguliwa.

Watu wengine tisa walikufa huko Santo Domingo, katika ajali tofauti ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa ukuta wa nyumba.

Mtu mmoja alisombwa na maji katika jimbo la San José de Ocoa (kusini) huku vifo vingine viwili vikitokea katika hali kama hiyo katika jimbo la La Altagracia (mashariki). Baadhi ya watu 13,000 walihamishwa kutoka maeneo hatarishi, kulingana na COE.

Rais wa Dominika Luis Abinader alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumapili kwamba ilikuwa "mvua kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika Jamhuri ya Dominika." Alitangaza kuwa masomo yamesitishwa hadi Jumatano ili "kuhakikisha usalama wa watoto na vijana".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.