Pata taarifa kuu
MVUTANO-UHASAMA

Mvutano waibuka kati ya India na Canada, nchi zote mbili zawafukuza wanadiplomasia

Kufuatia mauaji ya Hardeep Singh Nijjar, kiongozi wa Sikh na raia wa Canada, nchini Canada mwezi Juni mwaka jana, Justin Trudeau amehusisha New Delhi katika mauaji haya. Mwanadiplomasia wa India alifukuzwa nchini jana Jumatatu. Na Jumanne hii, Septemba 19, India, kwa upande wake, iliamuru kufukuzwa kwa mwanadiplomasia mkuu wa Canada na kuelezea mashtaka ya Ottawa kama "upuuzi." Mahusiano kati ya nchi hizi mbili tayari yalikuwa machungu, yanazidi kuwa ya wasiwasi.

Bango likiwa nje ya Hekalu la Guru Nanak Sikh Gurdwara linaonekana baada ya kuuawa kwa kiongozi wa Sikh Hardeep Singh Nijjar ndani ya uwanja wa hekalu mnamo Juni 2023, huko Surrey, Canada.
Bango likiwa nje ya Hekalu la Guru Nanak Sikh Gurdwara linaonekana baada ya kuuawa kwa kiongozi wa Sikh Hardeep Singh Nijjar ndani ya uwanja wa hekalu mnamo Juni 2023, huko Surrey, Canada. REUTERS - CHRIS HELGREN
Matangazo ya kibiashara

Baada ya shutuma za Canada, majibu ya India yalikuwa ya haraka, anasema mwandishi wetu huko New Delhi, Sébastien Farcis. India inafutlia mbali shutuma za Canada, zinazochukuliwa kuwa "upuuzi na zisizo kuwa na msingi", na inaunga mkono na kuheshimu kanuni za "demokrasia". "Sisi ni taifa la kidemokrasia na kujitolea kwa nguvu kwa utawala wa sheria," Wizara ya Mambo ya Nje ya India imesema katika taarifa.

New Delhi inakanusha kuwa imeamuru kuuawa kwa Hardeep Singh Nijjar, mwanaharakati wa uhuru wa Sikh, raia wa Canada anayechukuliwa kuwa mtu mwenye msimamo mkali anatetea kujitenga kwa eneo lake na anayetafutwa na mamlaka ya India. India inaona kuwa ni tuhuma ya uhalifu mbaya dhidi yake.

Baada ya kuitisha upinzani, Waziri Mkuu Justin Trudeau alitangaza jana kwamba kuna "ushahidi wa kuaminika kwamba kuna uwezekano wa uhusiano kati ya maafia wa Serikali ya India na mauaji ya Hardeep Singh Nijjar (kiongozi wa Sikh) , raia wa Canada" mwezi Juni mwaka huu. Inaaminika vya kutosha kwa hali yoyote sababu iliyoifanya Canada kumfukuza mwanadiplomasia mkuu wa India.

"Kuhusika kwa serikali yoyote ya kigeni katika mauaji ya raia wa Canada katika ardhi ya Canada ni ukiukaji usiokubalika wa uhuru wetu," Trudeau ameongeza. Dakika chache baadaye, Mélanie Joly, Waziri wake wa Mambo ya Nje, alitangaza kumfukuza mkuu wa shirika la kijasusi la India nchini Canada (RAW). "Madai kwamba mwakilishi wa serikali ya kigeni anaweza kuwa alihusika katika mauaji ya raia wa Canada hapa nchini Canada, katika ardhi ya Canada, sio tu yanatia wasiwasi, lakini hayakubaliki kabisa," alisema Mélanie Joly.

Mwanaharakati aliyekuwa akitafutwa na mamlaka ya India

Mwanaharakati wa kuundwa kwa jimbo la Sikh anayejulikana kama Khalistan, Hardeep Singh Nijjar alikuwa akisakwa na mamlaka ya India kwa madai ya vitendo vya kigaidi na njama ya kutekeleza mauaji. Mashtaka ambayo alikanusha, kulingana na Shirika la Sikh Ulimwenguni la Canada, shirika lisilo la kiserikali ambalo linadai kutetea masilahi ya Masingasinga wa Canada.

Tangu mauaji haya na maandamano yaliyofuata huko Canada, mvutano umeongezeka kati ya Ottawa na New Delhi. Serikali ya India inamtuhumu Justin Trudeau kwa kufumbia macho shughuli za watu wenye itikadi kali wa kitaifa wa Sikh ambao wanatetea kuundwa kwa jimbo huru la Sikh kaskazini mwa India.

Ottawa hivi majuzi ilisitisha mazungumzo ya makubaliano ya biashara huria na India na Waziri wa Biashara wiki iliyopita alifuta safari iliyopangwa kwenda nchini humo mnamo mwezi Oktoba. Siku ya Jumatatu Serikali ya Canada iliitaka serikali ya India "kushirikiana kufafanua suala hili", ikibainisha kuwa Justin Trudeau alizungumza na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati wa mkutano wa kilele wa G20, siku chache kabla.

Modi hakubaliani na fikra kutoka nje ya nchi kwa wanaotaka kujitenga

India mara nyingi imelalamika kuhusu shughuli za Walawi wanaoishi nje ya nchi, hasa nchini Canada, ambao kulingana na New Delhi wanaweza kufufua harakati za kujitenga kutokana na usaidizi mkubwa wa kifedha. Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, alielezea mapema mwezi eptemba "wasiwasi wake mkubwa juu ya kuendelea kwa shughuli dhidi ya India za watu wenye itikadi kali nchini Canada" wakati wa mkutano wake na Justin Trudeau, kwenye hafla ya mkutano wa mwisho wa G20 nchini India. Justin Trudeau kisha aliambia vyombo vya habari kwamba daima atatetea "uhuru wa kujieleza, uhuru wa dhamiri na uhuru wa kuandamana kwa amani", huku akichukua hatua dhidi ya chuki.

Jimbo la India la Punjab, ambalo lina karibu 58% ya watu kutoka jamii ya Sikh na 39% ya Wahindu, lilikumbwa na vuguvugu lenye vurugu la kutaka kujitenga katika miaka ya 1980 na mapema miaka ya 1990, ambapo maelfu waliuawa. Leo hii, wafuasi wengi wa vuguvugu hilo wanatoka hasa katika jimbo laPunjab. Canada ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Masingasinga nje ya jimbo lao la Punjab, India.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.