Pata taarifa kuu

Mahakama ya Argentina yaishutumu Iran kwa mashambulizi dhidi ya jumuiya ya Wayahudi

Mahakama ya Argentina iimeamua hivi punde siku ya Alhamisi jioni Aprili 11 kwamba mashambulio dhidi ya ubalozi wa Israeli mnamo mwaka 1992 na majengo ya Jumuiya ya Waisraeli ya Argentina (AMIA) mnamo mwaka 1994 huko Buenos Aires yalifadhiliwa na Irani, katika uamuzi uliotajwa kuwa wa "kihistoria" na Wayahudi wa eneo hilo, kwa mujibu wa vyombo vya habari na vyanzo vya mahakama. 

Shambulio dhidi ya Jengo la Mfuko wa Jamii ya Wayahudi AMIA huko Buenos Aires mwaka 1994 lilisababisha vifo vya watu 85.
Shambulio dhidi ya Jengo la Mfuko wa Jamii ya Wayahudi AMIA huko Buenos Aires mwaka 1994 lilisababisha vifo vya watu 85. REUTERS/Marcos Brindicci
Matangazo ya kibiashara

Shambulio la mwaka 1992 lilisababisha vifo vya watu 29 na shambulio la mwaka 1994 lilisababisha vifo vya watu 85, shambulio baya zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Uamuzi wa Mahakama ya Shirikisho pia unalitaja vuguvugu la Kishia la Hezbollah kuwa wahusika wa shambulio hilo, na kutangaza Iran kuwa "nchi ya kigaidi" na kuelezea shambulio dhidi ya AMIA kama "uhalifu dhidi ya ubinadamu".

"Hezbollah ilifanya operesheni ambayo ilijibu madhumuni ya kisiasa, kiitikadi, mapinduzi na chini ya mamlaka ya serikali, ya nchi," Jaji Carlos, mmoja wa majaji watatu waliochukuwa uamuzi huo, ameiambia Radio Con Vos, akimaanisha Iran.

Hukumu ya "kihistoria"

Tangazo la majaji hao linakuja kama sehemu ya utaratibu sambamba na mashambulizi yenyewe, kufuatia rufaa ya kuhukumiwa kwa kuzuia uchunguzi, kwa upande wa jaji na mkuu wa zamani wa upelelezi.

Hata hivyo majaji wamethibitisha kwamba msukumo wa mashambulizi hayo mawili, ingawa ni mengi, ulijibu sera ya kigeni ya rais wa Peronist (kiliberali) wa wakati huo, Carlos Menem (1989-1999).

"Mashambulizi haya yana chimbuko hasa katika uamuzi wa upande mmoja wa serikali, uliochochewa na mabadiliko ya sera ya kigeni ya nchi yetu kati ya mwisho wa mwaka 1991 na katikati ya mwaka 1992, kufuta mikataba mitatu ya usambazaji wa nyenzo na teknolojia ya nyuklia iliyohitimishwa na Iran,” inasema hukumu sambamba, ambayo inabainisha makosa yaliyofanywa wakati wa uchunguzi, kulinganana shirika la habari la AFP, ambalo limepata kopi ya uamuzi.

Hukumu hiyo "ni ya kihistoria, ya kipekee nchini Ajentina, tuliidai sio tu Argentina: tulidaiwa na wahanga," amesema Jorge Knoblovitz, kiongozi wa ujumbe wa vyama vya Wayahudi vya Argentina, kwenye televisheni ya LN+. Aidha, "inafungua uwezekano wa malalamiko kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kwa sababu imethibitishwa wazi kwamba taifa la Iran ni taifa la kigaidi," ameongeza.

Shambulio dhidi ya AMIA halikuwahi kudaiwa au kufafanuliwa, lakini vyombo vya sheria vya Argentina na Israel tayari vilizingatia kuwa Iran ndio mfadhili na kwamba lilifanywa na wanachama wa Hezbollah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.