Pata taarifa kuu

Brazil: Takriban watu tisa wamefariki katika ajali ya basi na wengine wengi kujeruhiwa

Ajali ya basi ilisababisha vifo vya takriban watu tisa na zaidi ya ishirini kujeruhiwa siku ya Alhamisi katika jimbo la Bahia nchini Brazili (kaskazini-mashariki), kulingana na Polisi ya barabarani ya Shirikisho (PRF).

Basi, ambalo liliondoka Rio de Janeiro (kusini-mashariki) kuelekea Porto Seguro, mji wa kitalii kusini mwa jimbo la Bahia, liliacha njia na kupinduka mwendo wa saa10 Alfajiri (saa 2 mjini Paris), imesema PRF, ikibainisha kuwa watu 34 walikuwa kwenye gari hilo.
Basi, ambalo liliondoka Rio de Janeiro (kusini-mashariki) kuelekea Porto Seguro, mji wa kitalii kusini mwa jimbo la Bahia, liliacha njia na kupinduka mwendo wa saa10 Alfajiri (saa 2 mjini Paris), imesema PRF, ikibainisha kuwa watu 34 walikuwa kwenye gari hilo. AFP - PABLO PORCIUNCULA
Matangazo ya kibiashara

Basi, ambalo liliondoka Rio de Janeiro (kusini-mashariki) kuelekea Porto Seguro, mji wa kitalii kusini mwa jimbo la Bahia, liliacha njia na kupinduka mwendo wa saa10 Alfajiri (saa 2 mjini Paris), imesema PRF, ikibainisha kuwa watu 34 walikuwa kwenye gari hilo.

Madereva wawili wa basi wko salama salimini

Kwa mujibu wa polisi, mwendo kasi unaweza kuwa chanzo cha ajali hiyo. Mamlaka haikutoa maelezo juu ya hali ya afya ya waliojeruhiwa, wala juu ya uraia wa waathiriwa.

Madereva hao wawili wa basi hawakujeruhiwa, kwa mujibu wa chanzo kimoja. Picha zilizorushwa kwenye vyombo vya habari vya ndani zinaonyesha basi nyeupe na buluu likiwa limelala kando ya barabara kuu ya BR-101.

Ajali za basi hutokea mara kwa mara nchini Brazili, nchi yenye viwango vya bara ambapo usafiri wa reli haujaendelezwa sana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.