Pata taarifa kuu

Idadi ya vifo kufuatia mkasa wa moto Hawaii yazidi 100

Idadi ya vifo kutokana na moto mbaya ambao karibu uteketeze mji mzima katika kisiwa cha Maui sasa inazidi watu 100, ametangaza gavana wa visiwa vya Marekani vya Hawaii, Josh Green. "Kufikia sasa watu 101 ndio wamefariki kufuatia mkasa wa moto," amesema katika hotuba yake ya televisheni, na kuongeza kuwa waokoaji sasa wametafuta zaidi ya robo ya eneo la tukio. Mamlaka inahofia kwamba huenda idadi hio ikaongezeka.

Idadi ya vifo kutokana na moto katika jimo la Hawaii imefikia watu 100.
Idadi ya vifo kutokana na moto katika jimo la Hawaii imefikia watu 100. © Mike Blake, Reuters
Matangazo ya kibiashara

Moto ulioteketeza kisiwa cha Maui, katika visiwa vya Hawaii, sasa ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea katika zaidi ya karne moja nchini Marekani, huku vifo 101 vimeorodheshwa, kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka kwa gavana wa Hawaii. Lakini takwimu bado inaweza kupanda, kwa sababu waokoaji wametafuta tu zaidi ya robo ya eneo la tukio.

Mji wa Lahaina, kwenye pwani ya magharibi ya Maui ulikuwa karibu kuteketezwa na moto huo. Papo hapo, maelfu ya majengo yameharibiwa na mengi yamekuwa rundo la majivu.

Mji mkuu wa zamani wa ufalme wa Hawaii, ambao ulikuwa na wakazi 12,000, sasa umeteketea na mamlaka tayari imeonya kwamba idadi ya watu bado inaweza kuongezeka kwa kiasi kikubwa katika siku chache zijazo.

Ndugu na jamaa za watu waliopotea wanahimizwa kupima damu zao, DNA, ili kusaidia kutambua maiti, ambazo mara nyingi hazitambuliki.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.