Pata taarifa kuu

Hitilafu ya mitambo ya kudhibiti safari za anga: Safari za anga zasitishwa kwa muda Marekani

Nchini Marekani, kwa saa kadhaa safari za ndege za ndani zilisitishwa kufuatia hitilafu iliyoripotiwa katika mfumo wa kitaifa wa kudhibiti safari za angaa nchini humo. 

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy mjini New York.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy mjini New York. Fuente: Reuters.
Matangazo ya kibiashara

Hitilafu hiyo ilisababisha mamlaka inayohusika na safari za ndege nchini humo, kuwatahadharisha marubani kutoanzisha safari zozote, kwa kuhofia hatari inayoweza kutokea katika njia ya ndege. 

Rais Joe Biden amearifiwa kuhusu kilichotokea, na Ikulu ya Marekani ikatao taarifa ikisema, hakuna ushahidi kuwa mfumo wake umeshambuliwa. 

Hitilafu hiyo, imechelewesha safari za ndege 760 ndani ya nje ya Marekani kuanzia Jumatano asubuhi, huku watalaam wakisema walikuwa wanafanya kila kinachowezekana kurejesha safari hizo. 

Abiria waliokuwa wasafari katika maeneo mbalimbali nchini Marekani, wamekwama katika viwanja vya ndege, huku wale waliopanga kusafiri wakishauriwa kupata taarufa kutoka kwa mashirika ya ndege kabla ya kwenda katika uwanja wa ndege. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.