Pata taarifa kuu

Brazili: Rais Lula atoa heshima za mwisho kwa kuaga mwili wa Pele

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva ametoa heshima zake za mwisho kwa Pele Jumanne, Januari 3, mbele ya jeneza la mwanasoka huyo nguli katika uwanja wa Santos.

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akimpa rambirambi Marcia Aoki, mjane wa marehemu mchezaji wa kandanda wa Brazil Pelé, katika uwanja wa Vila Belmiro huko Santos, Brazili, Jumanne, Januari 3, 2023.
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akimpa rambirambi Marcia Aoki, mjane wa marehemu mchezaji wa kandanda wa Brazil Pelé, katika uwanja wa Vila Belmiro huko Santos, Brazili, Jumanne, Januari 3, 2023. AP - Andre Penner
Matangazo ya kibiashara

Helikopta nyeupe ya rais imetua katika uwanja karibu na ule wa Vila Belmiro. Lula ameandamana na makamu wake wa rais Geraldo Alckmin, wanaripoti waandishi wetu maalum Annie Gasnier na Richard Riffoneau. Lula, ambaye alichukua wadhifa huo Jumapili mjini Brasilia, alitoa rambirambi zake kwa mjane wa Pele alipofika sehemu ambapo jeneza la Pelé limewekwa, katika uwanja ambao "Mfalme" wa soka alitamba akiwa na jezi ya Santos FC.

Wageni wa mwisho wameruhusiwa kwenye eneo hilo, lakini sasa ni wakati wa familia na wapendwa wa mwanasoka huyo mashuhuri kuja kutoa heshima zao za mwisho. Jeneza lake limezungukwa na mkewe Marcia Aoki, watoto wake, hasa Enthino, mwanasoka wa zamani ambaye anafanana sana na baba yake, hatimaye wajukuu na marafiki wapo katika uwanja huo wakitoa heshima zao za mwisho kwa "Mfalme" huyo wa soka.

Jeneza kupitishwa mbele ya nyumba ya mamake

Misa itafanyika hivi karibuni. Makaburi hayako mbali sana, ni kilomita moja tu kutoka uwanja wa Santos. Lakini msafara wa mazishi utazunguka mitaa ya Santos, utasimama mbele ya nyumba ya mama yake, Dona Celeste, mwenye umri wa miaka 100, kabla ya kufikishwa mahali pake pa kupumzika.

Siku ya Jumatatu, maelfu ya mashabiki, lakini viongozi wachache wa sasa wa soka, ikiwa ni pamoja na rais wa shirikisho la Soka Duniani, FIFA, Gianni Infantino, walikusanyika mbele ya jeneza jeusi la Pele lililowekwa katikati ya uwanja wa FC Santos, klabu ambayo alicheza kuanzia mwaka 1956 hadi 1974.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.