Pata taarifa kuu

Pele: Gwiji wa soka wa Brazil afariki akiwa na umri wa miaka 82

Nyota wa soka wa Brazil Pele, amefariki jana Alhamisi akiwa na umri wa miaka 82. Pele ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea duniani. Alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo na kibofu katika miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo familia yake inasema Pele amekuwa akiugua saratani ya utumbo.

Mchezaji pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu, akinyakua taji hilo mnamo 1958, 1962 na 1970, Pele alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Karne wa Fifa mnamo 2000.
Mchezaji pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu, akinyakua taji hilo mnamo 1958, 1962 na 1970, Pele alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Karne wa Fifa mnamo 2000. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Pele alikuwa akifanyiwa tiba ya kemikali tangu alipoondolewa uvimbe kwenye utumbo wake mnamo Septemba mwaka 2021.

Edson Arantes do Nascimento, anayejulikana zaidi kama Pele anasifiwa kwa kufunga mabao 1,281 katika rekodi ya dunia katika mechi 1,363 katika kipindi cha miaka 21 ya maisha yake.

Pele alishinda Kombe la Dunia mara tatu, akinyakua taji hilo mnamo 1958, 1962 na 1970, na alitangazwa kuwa mchezaji bora wa Karne wa Fifa mnamo 2000.

Risala za rambi rambi zinaendelea kumiminika kutoka kile pembe ya dunia- kuanzia fani ya michezo, siasa, burudani, sanaa na tamaduni, kwa mtu maarufu aliyeiweka Brazil katika ramani ya soka duniani.

Serikali yatangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa

Serikali ya Rais Jair Bolsonaro, anayeondoka madarakani mnamo siku ya Jumapili, imetangaza siku tatu za maombolezo, na kusema katika taarifa kuwa Pele alikuwa mzalendo halisi, akiliinua jina la Brazil kila mahali alipokwenda.

Mrithi wa Bolsonaro, Rais mteule Luiz Inacio Lula da Silva, ameandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa, "Wabrazil wachache sana wamefanikiwa kulibeba jina la nchi yetu kama alivyofanya Pele."

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema urithi wa Pele katika soka utaishi milele. "Mchezo. Mfalme. Milele," Macron aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter.

Mazishi yatafanyika kwenye Ukumbusho wa Necrópole Ecumênica, kaburi la wima huko Santos. Familia pekee ndiyo itahudhuria. Pelé ana nyumba huko Santos, ambako aliishi zaidi wakati wa uhai wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.