Pata taarifa kuu

Brazil: Jair Bolsonaro aondoka nchini kabla ya kukabidhi madaraka kwa Lula

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro aliondoka Brazil kuelekea Marekani siku ya Ijumaa, siku moja kabla ya kumalizika kwa muhula wake na kutawazwa kwa mrithi wake Luiz Inácio Lula da Silva huko Brasilia, vyombo vya habari kadhaa vimeripoti. Kiongozi huyo wa mrengo wa kulia tayari alikuwa ameonyesha mara kadhaa kwamba huenda hatakuwepo kwa zoezi la kukabidhi madaraka.

Kabla ya kuondoka Brazili, Rais anayemaliza muda wake Jair Bolsonaro alitoa hotuba kwenye mitandao ya kijamii, ambapo picha hii ilinaswa, mnamo Desemba 30, 2022, huko Brasilia.
Kabla ya kuondoka Brazili, Rais anayemaliza muda wake Jair Bolsonaro alitoa hotuba kwenye mitandao ya kijamii, ambapo picha hii ilinaswa, mnamo Desemba 30, 2022, huko Brasilia. © Présidence brésilienne / via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa hivyo hatakuwepo Jumapili Januari 1 kwenye sherehe ya kutambulishwa kwa rais mpya wa mrengo wa kushoto, mpinzani wake Lula da Silva, ambaye alitakiwa kumkabidhi kijiti cha urais kwa mujibu wa itifaki.

Akihojiwa na shirika la habari la AFP, rais hakutaka kuthibitisha habari hii. Makamu wa rais Hamilton Mourão anakaimu kama rais na atazungumza jioni ya Jumamosi Desemba 31, redio ya taifa RNR imetangaza.

Jair Bolsonaro ambaye yuko kimya sana tangu kushindwa katika uchaguzi wa urais, alizungumza na wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kuondoka kwake. Hasa, alilaani jaribio la shambulio lililoshindwa kabla ya Krismasi. Mhusika wa jaribio hili, mmoja wa wafuasi wake, alikiri kwanza kuhamasishwa na rais wa siasa kali za mrengo wa kulia, kabla ya kumtaja rais huyo.

Mwanachama wa kambi inayomuunga mkono Bolsonaro, aliweka kilipuzi kwenye lori la mafuta karibu na uwanja wa ndege wa Brasilia. Lengo: "kuchochea machafuko" na jeshi kuingilia kati.

Aondoka kuelekea Mar-o-Lago, kwa Donald Trump?

Bila kutaja kuondoka kwake kwenye mitandao, Jair Bolsonaro alipanda ndege ya jeshi la anga mwendo wa saa mbili usiku, saa za Brazil, viliripoti vyombo vya habari vya O Globo, CNN Brasil, Estadão na tovuti ya habari ya UOL.

"Niko kwenye ndege, nitarudi hivi karibuni," rais wa mrengo wa kulia amekiambia kituo cha CNN Brasil. Ikiwa Jair Bolsonaro hakuonyesha alikokuwa akienda, vyombo vyake vya usalama tayari viko Florida, Marekani. Mahali palipothibitishwa na gazeti la kila siku la Marekani la Washington Post.

Kulingana na vyombo vya habari vya Brazil, atakaa Mar-o-Lago, katika moja ya nyumba za rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, ambaye yuko karibu naye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.