Pata taarifa kuu

Marekani: Mashambulizi kwenye mitambo ya kuzalisha umeme husababisha matatizo

Nchini Marekani, mfululizo wa mashambulizi yamelenga mitambo ya kuzalisha umeme katika wiki za hivi karibuni, na kusababisha maelfu ya watu kukosa umeme kwa muda. Mashambulizi yanayoonyesha kuathirika kwa mitambo hii ya kimkakati.

Wafanyakazi wanakarabati Kituo cha Kuzalisha umeme cha Eastwood huko West End, North Carolina mnamo Desemba 6, 2022. Miundombinu iliharibiwa.
Wafanyakazi wanakarabati Kituo cha Kuzalisha umeme cha Eastwood huko West End, North Carolina mnamo Desemba 6, 2022. Miundombinu iliharibiwa. AP - Travis Long
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya - zaidi ya kumi - yalifanyika katika majimbo kadhaa: Oregon, North Carolina na hivi karibuni katika Jimbo la Washington. FBI (Shirika la Upelelezi la Marekani) linafanya uchunguzi. Kufikia sasa, hakuna mshukiwa ambaye ametambuliwa au kukamatwa. Na mamlaka zinasema bado hazijaweza kujua kama haya ni mashambulizi yaliyoratibiwa.

Lakini matukio haya yanazua hofu ya "aina mpya ya tishio", kulingana na Roy Cooper, gavana wa North Carolina. Kwa sababu mitambo ya umeme, kwa sehemu kubwa, iko hatarini sana. Inalindwa tu na ukuta, vizuizi au waya yenye miinuko ambayo ni rahisi kukwepa.

Tishio la makundi ya mrengo wa kulia

Katika visa vingi vya uharibifu au mashambulizi, wahalifu wamekuwa wakirusha risasi dhidi ya transfomawakiwa mbali. Wakati mwingine chupa moja iliyotupwa juu ya vizuizi inatosha kusababisha uharibifu. Maafisa wanadai kuwa wameimarisha usalama wao katika miaka ya hivi karibuni, lakini hii bado haitoshi.

Ingawa hakuna ushahidi kwamba mashambulizi haya ya hivi majuzi yanahusishwa, wataalam wanasema wamekuwa wakionya mamlaka kwa miaka kadhaa dhidi ya tishio la makundi ya mrengo mkali wa kulia, ambao vikao vyao vya majadiliano huibua hali ya aina hii ili kuleta machafuko. Katika ripoti ya hivi majuzi, Wizara ya Usalama wa Taifa inathibitisha kwamba tishio hili ni la kweli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.