Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Washington yataka kuweka shinikizo kwa Beijing

Huku Moscow ikizidisha mashambulizi yake nchini Ukraine, huku hali inayoizunguka Mariupol inavyozidi kuwa mbaya kwa raia, Washington inajaribu mkakati mpya leo: ule wa kuongeza shinikizo kwa Beijing. Wanadiplomasia wawili wa China na Marekani wanakutana Jumatatu hii, Machi 14 mjini Roma, na Marekani inakusudia kuiambia China kutovuka mipaka kuhusu msaada wao kwa Urusi.

Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani, Jake Sullivan (picha yetu) ameionya Beijing kwamba China haiwezi kuisaidia Urusi kukwepa vikwazo vya kiuchumi bila madhara yoyote kwake.
Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani, Jake Sullivan (picha yetu) ameionya Beijing kwamba China haiwezi kuisaidia Urusi kukwepa vikwazo vya kiuchumi bila madhara yoyote kwake. AFP - ANDREW CABALLERO-REYNOLDS
Matangazo ya kibiashara

Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan aliionya Beijing siku ya Jumapili kupitia vyombo vya habari kwamba China haiwezi kuisaidia Urusi kukwepa vikwazo vya kiuchumi bila kupata madhara yoyote. Ili kuhalalisha tuhuma zake, utawala wa Biden uliambia gazeti kuu la kila siku la Marekani jana kwamba Urusi iliiomba China msaada na vifaa vya kijeshi hasa.

Jumbe

Hizi ndizo jumbe kuu ambazo Jake Sullivan atawasilisha kwa mshauri mkuu wa China, Yang Jiechi, mjini Roma hivi karibuni. Afisa hyo wa China atakuwa na chaguzi mbili: ile ya kuendelea kuonyesha kuwa kutoegemea upande wowote, kwa kujiweka mbali na Urusi kuhusu vita vya Ukraine ili kuwenda sambamba na Marekani na Ulaya, washirika wake wawili wa kibiashara.

"Mtazamo wa kiutaratibu wa dunia"

Au hata ule wa kufichua mchezo ambao Washington inazidi kuhofia: ule wa kuona China ikishirikiana na Urusi kwenye uvamizi wa Ukraine, wakitumai kwamba hii inakuza "maono ya kiutaratibu wa ulimwengu" ambayo Beijing ingependa kuona umetatuliwa kwa muda mrefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.