Pata taarifa kuu

Jamhuri ya Dominika yazindua ujenzi wa ukuta kwenye mpaka na Haiti

Rais wa Jamhuri ya Dominika, Luis Abinader, alizindua Jumapili, Februari 20, kwa shangwe kubwa ujenzi wa ukuta wa kilomita 160 kwenye mpaka wa nchi yake na Haiti. Mradi wenye utata ambao, kulingana na rais huyo, unapaswa kusaidia "kudhibiti" uhamiaji haramu na uhalifu.

Rais wa Jamhuri ya Dominika, Luis Abinader, amezindua ujenzi wa ukuta wa kilomita 160 kwenye mpaka wa nchi yake na Haiti.
Rais wa Jamhuri ya Dominika, Luis Abinader, amezindua ujenzi wa ukuta wa kilomita 160 kwenye mpaka wa nchi yake na Haiti. Erika SANTELICES AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Kizuizi hiki "kitanufaisha nchi zote mbili, kwani kitawezesha kudhibiti biashara ya nchi mbili kwa ufanisi zaidi, kudhibiti wimbi la wahamaji kwa kupambana dhidi ya biashara ya magendo ya binadamu, kupambana dhidi ya biashara ya dawa za kulevya na uuzaji haramu wa silaha," Luis Abinader alisema wakati wa sherehe katika eneo la mpaka wa Dajabon kaskazini magharibi.

Luis Abinader ambaye alichaguliwa mnamo 2020, ambaye vita dhidi ya uhamiaji haramu ni moja ya malengo yake makuu - aliahidi kujenga ukuta huu mwaka mmoja uliopita. Kazi hiyo itagharimu dola milioni 31 na itadumu kwa miezi tisa.

Hatua ya kwanza, iliyozinduliwa Jumapili, itakuwa na kilomita 54 za uzio "katika maeneo yenye watu wengi na nyeti ya mpakani", kulingana na rais. Hatua ya pili itapanua ukuta hadi kilomita 110. Kwa hivyo ukuta huo utapima zaidi ya kilomita 164 kati ya 380 za mpaka kati ya majirani wawili wanaoshiriki kisiwa cha Hispaniola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.