Pata taarifa kuu
CANADA-USALAMA

Canada: Polisi yazindua operesheni kubwa kufungua barabara zilizozuiliwa Ottawa

Polisi ya Canada imetangaza kwamba imeanzisha operesheni kubwa ya kufungua barabara za mji wa Ottawa. Mji mkuu wa shirikisho umedumazwa kwa karibu wiki tatu na waandamanaji wanaopinga hatua za kiafya.

Polisi wa Canada wakijiandaa kuingilia kati dhidi ya waandamanaji wanaopinga hatua za afya wakifunga barabara za mji mkuu wa shirikisho Ottawa.
Polisi wa Canada wakijiandaa kuingilia kati dhidi ya waandamanaji wanaopinga hatua za afya wakifunga barabara za mji mkuu wa shirikisho Ottawa. © Robert Bumsted/AP
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa polisi, ambao walitumwa kwa wingi katika mitaa ya mji mkuu wa shirikisho, wameanza kukamata watu kuanzia Ijumaa saa mbili asubuhi saa za nchini Canada, kulingana na sirika la habari la AFP. Katika ukurasa wake wa Twitter, polisi imewasihi tena "waandamanaji kuondoka mara moja" na kuwataka kuwa "watulivu".

Polisi "inataka kuwashauri kwamba chini ya sheria ya mkoa na shirikisho, mtakabiliwa na adhabu kali ikiwa hamtasitisha shughuli zenu zisizo halali na kutoondoa magari na mali zenu mara moja kutoka maeneo yote ya maandamano haramu" imebaini.

Alhamisi jioni, polisi iliwakamata kundi la kwanza la watu, ikiwalenga hasa waliohusika na harakati. Tamara Lich, mmoja wa waandaaji wa msafara huo, alikamatwa na polisi.

Kufungwa kwa Baraza la Wawakilishi

Baraza la Wawakilishi la Canada lilifungwa siku ya Ijumaa kwa sababu za kiusalama. "Bunge la Wwawakilishi lilitarajia kuanza tena mjadala leo juu ya matumizi ya sheria ya dharura. Kufuatia mapendekezo ya usalama wa Bunge, Spika na viongozi wa Baraza la vyama vyote wamekubaliana kufuta kikao cha leo,” amesema Mark Holland, Kiongozi wa Serikali katika Baraza la Wawakilishi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.