Pata taarifa kuu

Marekani: Aliyekuwa rais wa Bunge la Seneti Harry Reid aaga dunia

Aliyekuwa rais wa Bunge la Seneti la Marekani, Harry Reid, mwanasiasa mashuhuri katika Chama cha Democratic na katika siasa nchini Marekani kwa miongo kadhaa, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82, mkewe ametangaza.

Aliyekuwa rais wa Bunge la Seneti kutoka chama cha Democraetic Harry Reid, huko Capitol Hill mwaka 2012.
Aliyekuwa rais wa Bunge la Seneti kutoka chama cha Democraetic Harry Reid, huko Capitol Hill mwaka 2012. AP - J. Scott Applewhite
Matangazo ya kibiashara

"Alifariki dunia mchana wa Jumanne," mke wa Harry Reid alisema katika taarifa, akiongeza kwamba kifo hicho kilifuatia vita vya miaka minne dhidi ya saratani ya kongosho.

Kiongozi wa wengi katika Bunge la Seneti kati ya mwaka 2007 na 2015, seneta Harry Reid alikuwa mtu muhimu mwishoni mwa utawala wa George W. Bush, na sehemu kubwa ya mihula miwili ya Barack Obama.

Uzoefu wake katika huduma ya Obamacare

Harry Reid alikuwa ametumia uzoefu wake wa muda mrefu katika Bunge la Congress kumsaidia rais kutoka chama cha Democratic, Barack Obama, kupitisha mageuzi yake ya matibabu ya Obamacare, moja ya miradi muhimu ya kisheria katika miaka yake minane katika Ikulu ya White House.

Harry Reid alizaliwa na kukulia katika mji mdogo wa uchimbaji madini wa Searchlight, Nevada Magharibi mwa Marekani, katika nyumba isiyo na maji ya bomba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.