Pata taarifa kuu
HAITI-USALAMA

Haiti: Raia 12 wa kigeni waliotekwa nyara mwezi Oktoba waachiliwa

Kundi la watekaji nyara limewaachilia raia 12 wa mwishio wa kigeni Alhamisi hii Desemba 16 waliotekwa nyara miezi miwili iliyopita na familia zao, Wamarekani 11 na raia mmoja wa Canada. Kwa jumla, watu 17 walitekwa nyara mwezi Oktoba.

Genge la "Mawozo 400", mojawapo ya ya magenge yenye nguvu zaidi nchini, lilidai dola milioni 17 ili waachiliwe. Mwishoni mwa mwezi Oktoba, katika video, kiongozi wa genge hilo alitishia kuwanyonga.
Genge la "Mawozo 400", mojawapo ya ya magenge yenye nguvu zaidi nchini, lilidai dola milioni 17 ili waachiliwe. Mwishoni mwa mwezi Oktoba, katika video, kiongozi wa genge hilo alitishia kuwanyonga. AFP - RICARDO ARDUENGO
Matangazo ya kibiashara

Miezi miwili iliyopita, watu wazima kumi na wawili na watoto watano, akiwemo mtoto mchanga, walitekwa nyara katika kitongoji vya Port-au-Prince - Wamarekani 16 na raia mmoja wa Canada. Watu hao ni kutoka dhehebu la kidini la Christian Aid Ministries, lililoko Marekani, na walikuwa wakirejea kutoka katika kituo cha watoto yatima kilichoko kilomita 30 mashariki mwa mji mkuu wa Haiti - katika eneo linalochukuliwa kuwa hatari sana.

Genge la "Mawozo 400", mojawapo ya ya magenge yenye nguvu zaidi nchini, lilidai dola milioni 17 ili waachiliwe. Mwishoni mwa mwezi Oktoba, katika video, kiongozi wa genge hilo alitishia kuwanyonga.

Lakini mwezi mmoja baadaye zoezi la kuwaachilia lilianza, hatua kwa hatua, kwanza watu wawili mwishoni mwa mwezi Novemba, kisha watatu mapema mwezi Desemba. Marekani ilikuwa imesema inashirikiana na serikali ya Haiti na Canada kuhakikisha kuwa mateka hao wameachiliwa. Kumi na mbili wa mwisho wameachiliwa leo.

Hii ni mara ya kwanza kwa mateka wa kigeni kushikiliwa kwa muda mrefu nchini humo. Raia wa Haiti wameteseka kwa miezi kadhaa visa hivi vya utekaji nyara, kutokana na kuongezeka kwa magenge yenye silaha nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.