Pata taarifa kuu
COLOMBIA-USALAMA

Colombia: Rais Duque atuma jeshi Cali baada ya maandamano ya mwezi mmoja

Baada ya mwezi mmoja wa maandamano ya raia wenye hasira nchini Colombia, Rais wa nchi hiyo Ivan Duque amemuru kupelekwa kwa jeshi katika mitaa ya Cali, kitovu cha maandamano.

Mwanajeshi akiwa na waandamanaji huko Cali ambapo rais wa Colombia amepeleka jeshi, Mei 28, 2021.
Mwanajeshi akiwa na waandamanaji huko Cali ambapo rais wa Colombia amepeleka jeshi, Mei 28, 2021. AFP - LUIS ROBAYO
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Colombia ametangaza kupelekwa kwa jeshi huko Cali na katika maeneo yote ya Valle del Cauca. Mji huu wa tatukwa ukumbwa nchini Colombia ni kitovu cha maandamano ya raia ambayo yamedumu mwezi mmoja.

"Kuanzia usiku huu tunaanza kupeleka idadi kubwa ya wanajeshi kuchukuwa nafasi ya maafisa wa polisi katika jiji la Cali", ameagiza Rais Ivan Duque ambaye aliongoza kikao cha baraza la usalama katika jiji hilo lenye wakazi milioni 2.2 jana Ijumaa.

"Tutapeleka idadi kubwa, karibu mara tatu ya maafisa waliokuwepo hapo kabla, chini ya masaa 24, pia tutazidisha ulinzi katika maeneo muhimu ambapo tumeshuhudia vitendo vya uharibifu, vurugu na ugaidi wa mijini wenye nguvu ndogo," amebaini.

Angalau watatu wapoteza maisha

Maandamano mapya yamesababisha vifo vya watu watatukatika mji huo, ikiwa ni pamoja na mchunguzi kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka wa Cali ambaye alifyatua risasi kwenye umat wa watu, na kuua raia mmoja, kabla ya kuuawa kwa kupigwa mawe na waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.