Pata taarifa kuu
MAREKANI-OBAMA-SIASA-USALAMA

Marekani: Obama aendelea kumshambulia Donald Trump

Ikiwa imsalia wiki moja kabla ya uchaguzi wa rais nchini Marekani, rais wazamani wa nchi hiyo Barack Obama anaendelea na kampeni kwa niaba ya makamu wake wa zamani Joe Biden.

Rais wa zamani Barack Obama akizungumza katika mkutano kwa niaba ya Biden huko Orlando, Florida, Oktoba 27, 2020.
Rais wa zamani Barack Obama akizungumza katika mkutano kwa niaba ya Biden huko Orlando, Florida, Oktoba 27, 2020. AP Photo/John Raoux
Matangazo ya kibiashara

Katika kampeni yake huko Orlando, Florida Jumanne wiki hii, Barack Obama alilaumu usimamizi wa Donald Trump katika mapambano dhidi ya janga la COVID-19.

Barack Obama alizungumza mbele ya magari, na badala ya kushangilia kwa kupiga makofi, wafuasi wake ambao walikuwa wamekuja kumsikiliza huko Orlando amekuwa wakipiga honi wakati wowote anapomshambulia Donald Trump kwa jinsi anavyoshughulikia janga ambalo mrithi wake amemkosoa vikali.

"Siku nyingine kwenye mkutano alisema kwamba watu wanatilia maanani sana COVID-19. Huenda alikuwa na wivu kuona jinsi taarifa mbalimbali kuhusu ugonjwa huo hatari zikirushwa kwenye vyombo vya habari! Kauli aliyotumia sio sahihi kwa kiongozi kama yeye, " amesema barack Obama.

Shtuma kama hizo hazijawahi kutokea katika nchi ambayo ni kawaida kwa rais wa zamani kutomkosoa mrithi wake. Lakini baada ya kukaa kimya kwa mashambulizi ya Donald Trump kwa karibu miaka minne, Barack Obama ameamua kuvunja utamaduni huo katika siku za mwisho za kampeni.

Kampeni hiyo ilirushwa moja kwa moja na vituo vyote vya habari, hata kituo cha Fox News kilicho karibu na Donald Trump kilirusha kampeni hiyo.

Hii ni kampeni ya tatu ya Barack Obama kwa kumuunga mkono makamu wake wa zamani. Lengo sio kukusanya wapiga kura wapya bali kuhamasisha wapiga kura wa chama cha Democratic. Lazima mwende kupiga kura, msiwe wavivu kama mwaka 2016 ili tuweze kumuangusha Donald Trump, amesema Obama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.