Coronavirus: Zaidi ya visa vipya 12,000 vyathibitishwa Brazil
Brazil imerekodi visa vipya 12,342 vilivyothibitishwa vya virusi vya Corona na vifo vipya 290 vilivyohusishwa na janga hilo katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, wizara ya afya imesema.
Imechapishwa:
Idadi ya visa vya maambukizi nchini Brazili inazidi milioni 5.0, na jumla ya vifo 150,488 sasa vimerekodiwa, kulingana na takwimu za serikali.
Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.
Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.