Pata taarifa kuu
BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya vifo vipya 1,000 vyathibitishwa nchini Brazil

Brazil imerekodi visa vipya 35,816 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo vipya 1,075 vinavyohusiana na janga hilo katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, Wizara ya Afya imeripoti.

Brazil ni nchi ya pili kuathirika zaidi na mgogoro wa kiafya baada ya Marekani, kwa suala la maambukizi au vifo.
Brazil ni nchi ya pili kuathirika zaidi na mgogoro wa kiafya baada ya Marekani, kwa suala la maambukizi au vifo. REUTERS/Ricardo Moraes
Matangazo ya kibiashara

Brazil imeripoti karibu visa milioni 4.2 vya maambukizi, na vifo 128,539 vimerekodiwa kwa jumla, kulingana na takwimu za serikali.

Brazil ni nchi ya pili kuathirika zaidi na mgogoro wa kiafya baada ya Marekani, kwa suala la maambukizi au vifo.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.