Pata taarifa kuu
MAREKANI-ICC-HAKi-USALAMA

Marekani yamuwewekea vikwazo mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameiita Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, kuwa ni taasisi "fisadi". Washington inalaani uchunguzi wa mahakama hiyo ya kimataifa unaolenga wanajeshi wa Marekani waliopelekwa nchini Afghanistan.

Mwendesha mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda, Januari 28, 2016.
Mwendesha mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda, Januari 28, 2016. ©ICC-CPI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ndiye alitangaza uamuzi huo ambao haujawahi kutokea. Mike Pompeo amesema ni "muhimu kuanza kuchukuwa hatua dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu".

"Leo tunaamua kuchukuwa hatua! Marekani haijawahi kutia saini kwenye Mkataba wa Roma uliounda mahakama hiyo ya kimataifa, na hatutavumilia vitimbi vyake visivyokubalika kuwaweka Wamarekani chini ya mamlaka yake, " ameongeza waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.

Washington imeamua kumuweka mwendesha mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda, na pia mmoja wa washirika wake Phakiso Mochochoko kwenye orodha nyeusi. Vikwazo vya kiuchumi pia vimechukuliwa dhidi yao. Hatua ambazo zinaweza pia kuathiri mtu yeyote ambaye anashirikiana na mwendesha mashtaka, amesema Mike Pompeo.

Mwezi Aprili mwaka huu Mwendesha mashtaka wa ICC alinyimwa visa kusafiri kwenda nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.