Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-CHANJO-CORONA-AFYA

Trump kuhamisha jeshi kupewa chanjo dhidi ya Covid-19

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza leo Alhamisi kwamba atahamasisha wanajeshi wa nchi hiyo, muda ukiwadia, kupewa chanjo dhidi ya Covid-19, huku akibaini kwamba wazee watapewa kipaumbele katika mpango huo kutoa wa chanjo.

Rais wa Marekani Donald Trump awali alilishutumu shirika la Afya Duniani, WHO, kwa kuipendelea China, baada ya kusema kuwa walipuuzia kuhusu hatari ya ugonjwa wa Covid-19..
Rais wa Marekani Donald Trump awali alilishutumu shirika la Afya Duniani, WHO, kwa kuipendelea China, baada ya kusema kuwa walipuuzia kuhusu hatari ya ugonjwa wa Covid-19.. MANDEL NGAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Unajua kuwa kutoa chanjo hii itakuwa kazi kubwa," amesema rais kwenye runinga ya Fox Busness Network.

"Jeshi letu sasa limehamasishwa ili mwisho wa mwaka, tuweze kutoa chanjo hiyo haraka sana kwa watu wengi, " ameongeza rais wa Marekani.

Hakuna chanjo ambayo iko tayari kwa sasa dhidi ya virusi vya ugonjwa wa SARS-CoV-2, lakini utafiti zaidi unaendelea, na Donald Trump amesema anaamini chanjo itakuwa tayari mwishoni mwa mwaka huu. Ni kwa mantiki hii Marekani iimeanza kuhamasisha vikosi vyake vya jeshi.

Watu Milioni 1.42 wameambukizwa virusi vya Corona, baada ya wagonjwa wapya 20,568 kuthibitishwa, huku wagonjwa 244,000 wamepona na watu 84,763 wamefariki dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.