Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Hali ya mvutano yaongezeka Marekani

Miji kadhaa ya Marekani inaendelea kukumbwa na maandamano, baada ya kuonekana ukosefu wa sera moja kuhusu kuondolewa kwa hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

Moja ya maeneo ya fukwe za Florida yamefunguliwa tena, Jumapili Aprili 19, 2020 huko Marekani.
Moja ya maeneo ya fukwe za Florida yamefunguliwa tena, Jumapili Aprili 19, 2020 huko Marekani. REUTERS/Sam Thomas
Matangazo ya kibiashara

Maandamano yameripotiwa jana Jumapili katika majimbo ya Arizona, Colorado, Montana na Washington, maandamano makubwa yakitarajiwa leo Jumatatu.

Marufuku ya kutokutoka nje ilikwa katika majimbo yote ya Marekani ili kudhibiti kusambaa kwa janga la Covid-19, hali iliyotikisa uchumi wa taifa hilo kubwa zaidi kiuchumi duniani

Kwa sasa kila Jimbo linatumia sheria zake katika suala la kukabiliana na kudhibiti janga hatari la Covid-19, na kusababisha mvutano zaidi na Ikulu ya White House.

Huko Florida, kwa mfano, Maeneo ya sharehe kwenye fukwe yamefunguliwa.

Picha za watu wakistarehe kwenye fukwe za Florida, zimeendelea kuzunguka mitandaoni na kwenye televisheni za Marekani tangu mwishoni mwa wiki hii. Mamia ya watu wakiwa kwenye maeneo ya fukwe huko Jacksonville. Baadi wa kitembea, wakimbia, wengine hwakiendesha baisikeli au kuogelea, bila kuheshimu sheria ya kutengana kwenye umbali wa mita moja au mbili. Florida inafungua tena maeneo ya starehe ya fukwe zake. Uamuzi uliotolewa na Gavana ukielezea kuwa watu wanahitaji mazoezi na hewa safi.

Huko Texas, Hifadhi ya Wanyama zimefunguliwa tena, wakati Gavana wa jimbo hilo anasema ana mpango wa kurejesha hali kawaida hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.