Pata taarifa kuu
NEW ZEALAND-UGAIDI-SILAHA

New Zealand yapiga marufuku silaha iliyotumiwa kuua watu 50 misikitini

New Zealand imetanagaza kupiga marufuku aina ya silaha iliyotumiwa kushambulia misikiti miwili mjini Christchurch na kusababisha vifo vya watu 50.

Waziri Mkuu wa New Zealand  Jacinda Arden.
Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Arden. AP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili limetolewa na Waziri Mkuu Jacinda Ardern ambaye amesema silaha aina hiyo haitanunuliwa tena nchini humo kutokana na kitendo hicho alichosema ni cha kigaidi.

Marufuku hayo yanatarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia tarehe 11 mwezi Aprili, baada ya  bunge kupitisha sheria hiyo.

Waziri Mkuu Ardern amesema, nchi hiyo haitabaki tena kama ilivyo, baada ya tukio hilo baya katika historia ya nchi hiyo.

‘Historia yetu imebadilika milele.Sheria zetu pia zimebadilika,’ alisema Waziri Mkuu Ardern.

Katika hatua nyingine, watu wote waliopoteza maisha, wameshambuliwa kwa mujibu wa ripoti za polisi.

Mshatakiwa wa shambulizi hilo ni raia wa Australia Brenton Tarrant, ambaye amefikishwa Mahakamani na kusema hajutii kutekeleza mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.