Pata taarifa kuu
MAREKANI-ISIL-USALAMA

Marekani yakataa Hoda Muthana kurejea nyumbani

Rais wa Marekani Donald Trump ameamua kukataa kurejea kwa Hoda Muthana nchini Marekani. Kwa mujibu wa serikali ya Marekani, Hoda Muthana ambaye alizaliwa New Jersey mwaka 1994 sio raia wa Marekani.

Hassan Shibly, mwanasheria wa Hoda Muthana, katika ofisi yake huko Tampa, Florida, Februari 20, 2019.
Hassan Shibly, mwanasheria wa Hoda Muthana, katika ofisi yake huko Tampa, Florida, Februari 20, 2019. Gianrigo MARLETTA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hoda Muthana ambaye alikwenda nchini Syria mnamo mwaka 2014, anazuiliwa katika kambi ya wapiganaji wa Kikurdi tangu kuanguka kusambaratika kwa kundi la Islamic State nchini Syria.

Hoda Muthana anataka kurudi katika nchi yake ya asili na kuonekana kwenye vyombo vya habari vya Marekani kama mtu aliyetubu dhambi.

Wakati ambapo kundi la Islamic State lilikuwa bado likishikilia maeneo yake, Hoda Muthana alikuwa akihusika kikamilifu katika propaganda ya kigaidi. Mnamo mwaka 2015, alipongeza kwenye ukurasa wake wa Twitter wahusika wa mauaji ya Charlie Hebdo, wakati huo akifahamika kwa jina la "Oum Jihadi". Lakini tangu kusambaratika kwa kundi la Islamic State, sasa Hoda Muthana anazuiliwa katika kambi ya wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria. Katika mahojiano na New York Times, Hoda Mutahana amesemakuwa tayari ametubu dhambi, na anataka kurejea nchini Marekani baada ya kuwa na pasipoti ya Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumatano wiki hii kwamba: "Nimetoa agizo kwa waziri wa mambo ya Nje Mike Pompeo kutoruhusu Hoda Muthana kurejea nchini Marekani. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.