Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-UCHUMI

Guaido: Msaada wa kibinadamu unatarajiwa kuingia Venezuela Februari 23

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela, Juan Guaido, ambaye hivi karibuni alijitangaza rais wa nchi hiyo, ametangaza kuwa msaada wa dharura kutoka Marekani utaingia nchini Venezuela tarehe 23 Februari licha ya rais Nicolas Maduro kukataa.

Kiongozi wa upinzani Juan Guaido aendelea kukabiliana na rais wa Venezuela Nicolas Maduro.
Kiongozi wa upinzani Juan Guaido aendelea kukabiliana na rais wa Venezuela Nicolas Maduro. REUTERS/Manaure Quintero
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni rais Maduro alikanusha kuwa nchi yake haikabiliwi na njaa.

Juan Guaido anasema hiyo itakuwa ni hatua ya kwanza kabla ya nchi yake kuingiliwa kijeshi.

"Tarehe 23 Februari, itakuwa siku ambapo msaada wa kibinadamu utaingia nchini Venezuela," Juan Guaido, ambaye anatambuliwa kama rais wa mpito na nchi zaidi ya hamsini, amesema mbele ya wafuasi wake katika eneo moja mashariki mwa Caracas.

"Nina uhakika kuwa msaada wa kibinadamu utaingia nchini Venezuela, kwa sababu huyu anayedai kuwa ni rais hana chaguo jingine ispokuwa tu kuondoka nchini Venezuela," amesema Juan Guaido, Spika wa bunge linalodhibitiwa na upinzani.

Ameomba watu 250,000 watakaojitolea kwa kusaidia katika kusafirisha misaada kutoka eneo inakofadhiliwa kwenye mpaka na Colombia hadi mjini Caracas, nchini Venezuela. Februari 23, itakuwa mwezi ni mmoja tangu Juan Guaido ajitangaze rais wa mpito wa Venezuela.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amemuonya mwenzake wa Marekani Mike Pompeo dhidi ya "matumizi yoyote ya nguvu" nchini Venezuela, wakati Washington ilisema iko tayari kuingilia kijeshi nchini Venezuela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.