Pata taarifa kuu
COLOMBIA-VENEZUELA-WAKIMBIZI

Colombia yahitaji msaada kwa kukabiliana na wimbi la wahamiaji

Colombia inasema inahitaji msaada wa kimataifa ili kukabiliana na wimbi la wakimbizi wa Venezuela ambao wanatoroka nchi yao kwa sababu za hali mbaya ya kiuchumi.

Wahamiaji wasio na makazi nchini Venezuela katika kituo cha michezo cha Cucuta, Colombia.
Wahamiaji wasio na makazi nchini Venezuela katika kituo cha michezo cha Cucuta, Colombia. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Rais Juan Manuel Santos, katika hotuba yake jana Jumanne, alisema "mfurahie msaada wa kifedha na misaada mbalimbali inayotolewa na jumuiya ya kimataifa".

"Tunahitaji misaada," aliongezea, "kwa sababu kwa bahati mbaya tatizo hili linazidi kuwa mbaya zaidi siku baada ya siku."

Serikali ya Colombia inabaini kwamba inalazimika kugharamia dola tano kwa siku na kwa kila mtu kulipia nyumba na chakula kwa wakimbizi wa Venezuela.

Wiki iliyopita Colombia iliimarisha udhibiti katika mpaka wake na Venezuela dhidi ya idadi kubwa ya raia wa Venezuela wanaoingia nchini humo kwa ktafuta maisha bora zaidi.

Idadi ya Venezuela nchini Colombia imeongezeka kwa 62% mwaka 2017 na kufikia watu karibu 550,000.

Wengi wao wanaishi katika mazingira mabaya katika miji iliyo kwenye mipaka, hasa katika mji mkubwa wa Cucuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.