Pata taarifa kuu
MAREKANi-MITANDAO YA KIJAMII-HABARI

Obama aonya dhidi ya mitandao ya kijamii

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ameonya kuhusu hatari ya matumizi ya mitandao ya kijamii, katika mahojiano na Prince Harry yaliyorushwa leo Jumatanokwenye kituo cha redio cha BBC Radio 4.

Picha ya Desemba 17, 2017 ya Prince Harry katika mahojiano naaliekua rais wa  Marekani Barack Obama.
Picha ya Desemba 17, 2017 ya Prince Harry katika mahojiano naaliekua rais wa Marekani Barack Obama. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Moja ya hatari za mtandao ni kwamba watu wanaweza kuona hali halisi tofauti kabisa, na kupata habari zinazokinzana," Obama amesema katika mahojiano hayo ya kwanza tangu kuondoka kwake madarakani mnamo mwezi Januari.

Alielezea wasi wasi kuhusu siku za usoni ambapo ukweli utapotoshwa na watu watakuwa wakisoma na kusikiliza vitu ambavyo vitakuwa vikiridhisha maoni yao.

Bw Obama alionya kuwa vitendo kama hivyo vinachanganya uelewa wa watu katika masuala magumu na kusambaza uvumi.

"Swali ambalo mtu anapaswa kujiuliza, vipi unaweza kutumia teknolojia hii ili kuruhusu wingi wa sauti, utofauti wa maoni, huku ukiepuka kuminya jamii," Barack Obama ameongeza, bila kutaja mrithi wake Donald Trump , anaekosolewa kwataarifa zake anazorusha kwenye twitter.

Barack Obama amesema wale walio katika nyadhifa za uongozi wanastahili kuwa waangalifu wakati wanaandika katika mitandao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.