Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-UN

Marekani yaitaka Korea kubadilika kabla ya kuingia kwenye meza ya mazungumzo

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson amesema Korea Kaskazini lazima ibadili njia zake kabla ya kuelekea katika meza ya mazungumzo , kauli ambayo inakinzana na ile ya awali ya Marekani kuwa tayari kwa mazungumzo bila masharti yoyote ili kukomesha mvutano na Pyongyang.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Tillerson ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kukomeshwa kwa tabia ya kudumu na ya kutisha ya Korea Kaskazini lazima kufanyike kabla ya kuanza kwa mazungumzo hasa baada ya kuwa chini ya shinikizo kutoka Ikulu ya Rais Donald Trump kumtaka kukaza msimamo wake.

Mapema wiki hii katika jukwaa la sera huko Washington, Tillerson alisisitiza kuwa Marekani ilikuwa inatafuta ufunguzi wa kidiplomasia wa mazungumzo na Korea ya Kaskazini ili kukomesha mpango wake wa nyuklia na, kwa mara ya kwanza, ilitoa nafasi ya mazungumzo bila ya masharti yoyote.

Ikulu ya White House ilijibu maneno ya Tillerson kwa kusisitiza kuwa hakuna mabadiliko katika sera ya Marekani, na kusababisha ripoti mpya ya kutofautiana kati ya Trump na mwanadiplomasia wake mkuu.

Kufuatia hali hiyo Tillerson mbele ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akachukua msimamo mgumu na kusisitiza kuwa wataendeleza kampeni kuhakikisha kuwa Korea Ksakazini inaachana na mpango wake wa silaha za nyuklia lakini akaongeza kuwa Marekani haihitaji wala haitafuti vita na Korea Kaskazini.

 

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.