Pata taarifa kuu
MAREKANi-USALAMA

Mjadala waibuka kuhusu matumizi ya silaha za nyuklia Marekani

Suala la matumizi ya silaha za nyuklia limeibua mjadala mkubwa nchini Marekani baada ya afisa wa ngazi ya juu katika jeshi, Jenerali Hyten, anayehusika na kuhifadhi silaha za nyuklia kutangaza kuwa atakataa kutekeleza agizo la Donald Trump ikiwa ataona kuwa ni kinyume na sheria.

Afisa wa jeshi la Marekani anaeongozana na rais katika safari zake akiwa na begi nyeusi liliomo sheia za nyuklia.
Afisa wa jeshi la Marekani anaeongozana na rais katika safari zake akiwa na begi nyeusi liliomo sheia za nyuklia. Olivier Douliery / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, kamati ya bunge la Senate ilijadili kuhusu mamlaka ya rais juu ya silaha za nyuklia. Jambo ambalo halijatokea tangu mwaka 1976.

Lakini Donald wa Trump anashikilia sheria za nyuklia: anaweza kuchukua uamuzi peke yake, na wabunge na maseneta kutoka vyama vyote wana wasiwasi. Katika mazingira ya mvutano unaoendelea na Korea Kaskazini, wengi wanahoji uwezo wa rais wa Marekani kufanya maamuzi muhimu, na kwa wakati mzuri.

Mwishoni mwa wiki hii iliyopita, Jeneral Hyten, anayehusika na kuhifadhi silaha za nyuklia, alitangaza kwamba atapinga agizo la Trump ikiwa ataona kuwa agizo hilo ni kinyume cha sheria. Lakini wataalamu wamesema kwamba rais ana uwezo wa kubadili mhusika wa silaha za nyuklia au hata kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha vita cha Pentagon (makao makuu ya jeshi) ili kutekeleza uamuzi wake.

Jenerali Hyten hataki kuhukumiwa kwa kutotii agizo lililo kinyume cha sheria, lakini hofu yake anapaswa kuijadili yeye binafsi. "Mlipuko wa atomiki utakua na madhara makubwa na hayatabiriki, " alisema Jenerali Hyten.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.