Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MAZUNGUMZO-USALAMA

Mazungumzo kati ya serikali ya Venezuela na upinzani yaendelea Santo Domingo

Wajumbe wa serikali ya Venezuela na upinzani wanaendelea Alhamisi hii nchini Jamhuri ya Dominika kuweka sawa ajenda ya mazungumzo ya kutatua mgogoro wa kisiasa unaoendelea kuikabili nchi yao, amesema Rais wa Jamhuri ya Dominika Danilo Medina.

Spika wa Bunge jipya la Katiba la Venezuela, Delcy Rodriguez (wa pili kutoka kushoto) na Jorge Rodriguez (kulia), kiongozi wa Chama cha Kisoshalisti cha kinachounga mkono serikali ya Venezuela, katika mkutano wa waandishi wa habari Santo Domingo, Dominika.
Spika wa Bunge jipya la Katiba la Venezuela, Delcy Rodriguez (wa pili kutoka kushoto) na Jorge Rodriguez (kulia), kiongozi wa Chama cha Kisoshalisti cha kinachounga mkono serikali ya Venezuela, katika mkutano wa waandishi wa habari Santo Domingo, Dominika. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tuko katika mchakato wa maendeleo, na kutengeneza ajenda inayoelekea kwa majadiliano ya mwisho ya mgogoro," amesema rais Madina, katika hutuba fupi kwa vyombo vya habari mwishoni mwa mkutano na wajumbe wote kutoka pande mbili husika katika mgogoo huo katika moja ya majengo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Dominika.

Mazungumzo yamepangwa kuanza tena Alhamisi hii saa 9:00 asubuhi saa za Jamhuri ya Dominika (sawa na saa saba kamili saa za kimataifa), rais Madina ameongeza.

"Kitu pekee ninachoweza kusema usiku wa leo ni kwamba tumesikiliza pande zote na wamejieleza na kutoa maoni yao juu ya hali inayoendelea nchini Venezuela," amesema rais wa Jamhuri ya Dominika, ambaye pia alikutana na waziri mkuu wa zamani wa Uhispania, José Luis Rodriguez Zapatero, mmoja wa waanzilishi wa majadiliano kati ya Wavenezuela.

Wawakilishi wa serikali ya Kisoshalisti ya Caracas na upinzani walikutana siku ya Jumatano katika Jamhuri ya Dominikai katika jaribio jipya la kutatua mgogoro mkubwa wa kisiasa.

Ujumbe wa rais Nicolas Maduo umesemakuwa una na matumaini makubwa kwa mazungumzo hayo.

"Naweza kusema kwamba tuko karibu sana na kutatua pointi nyingi ambazo ziko kwenye ajenda, na ambazo zitakua katika ajenda ya mazungumzo siku ya leo," Jorge Rodriguez, aliyetumwa na serikalikushiriki mazungumzo haya aliwahakikishi waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.