Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO

Trump na Putin walikutana mara mbili kwenye G20 nchini Ujerumani

Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin mara mbili pembezoni mwa mkutano wa G 20 wiki moja iliyopita.

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Marekani imesema ni kweli viongozi hao walikutana mara mbili lakini haikuweka wazi ni mambo gani ambayo viongozi hao waliyazungumzia.

Inaripotiwa kuwa, Trump na Putin walikutana kwa karibu saa mojana mtafsiri wao kwa siri pembezoni mwa mkutano huo wa G20.

Hata hivyo, rais Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter amekanusha madai kuwa mikutano hiyo ilikuwa ya siri kama vyombo vya Habari nchini Marekani vinavyoripoti.

Uhusiano kai ya Trump na Putin umekuwa ukithaminiwa na raia wa Marekani na wachambuzi wa siasa za Kimataifa kwa sababu ya madai kuwa, Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita na kumsaidia Trump kutangazwa mshindi.

Maafisa wa Inteljensia nchini Marekani wameendelea kuamini kuwa Urusi ilimsaidia Trump kushinda, madai ambayo rais Putin na Trump wamekanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.