Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Trump: Niko tayari kukutana na Kim Jong-Un

Rais wa Marekani Donald Trump alisema siku ya Jumatatu kuwa yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ikiwa hali itaruhusu, taarifa ambayo inakuja wakati ambapo Pyongyang imetishia kufanya jaribio la sita la nyuklia.

Rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House mjini Washington, Marekani, Machi 13, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House mjini Washington, Marekani, Machi 13, 2017. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Hali imeendelea kuzorota katika rais ya Korea katika miezi ya hivi karibuni kutokana na Pyongyang kuemndelea na mpango wake wa nyuklia na majaribio ya kurusha makombora ya masafa marefu.

Rais wa Marekani, ambaye alionyesha nia yake ya kuitumia China kwa kuishambulia korea Kaskazini hata hivyo alisema pia yuko tayari kutafutia suluhu peke yake tatizo hilo, ambapo anafikiria kukutana ana kwa ana na kiongozi wa Korea Kaskazini.

"Wanasiasa wengi kamwe hawawezi kusema hivyo, lakini mimi nasema kwamba kama hali itaruhusu, nitakutana naye. Nitalazimika kufanya hivyo," alisema Donald Trump katika mahojiano na shirika la habari la Bloomberg.

Muda mfupi baadaye, msemaji wake Sean Spicer, amepuuzia umuhimu wa taarifa hii, akisisitiza kwamba mkutano huo hauwezekani kwa sasa . "Itabidi abadili mara moja tabia yake mbaya ya uchokozi," Sean Spicer alisema.

Korea ya Kaskazini ilionya Jumatatu kuwa iko tayari kufanya "kwa wakati wowote" jaribio la sita la nyuklia.

Korea Kaskazini itaendelea kuimarisha uwezo wake wa "kuzuia mashambulizi ya nyuklia" kama Washington haitaachana na sera yake uchokozi, alisema msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Korea Kaskazini katika taarifa iliyorushwa ka shirika la habari la KCNA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.