Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-USAFIRI

Donald Trump kutoa agizo jipya kuhusu uhamiaji

Rais w aMarekani Donald Trump, wiki hii, labda Jumatano hii Februari 22, atatoa agizo jipya kuhusuuhamiaji, nakala itarejelea ile ya awali iliyozuiliwa na mahakama. Agizo hilo linapiga marufuku raia kutoka mataifa saba ya Kiislam kuingi nchini Marekani.

Wiki hii Donald Trump atatoa agizo jipya kuhusu uhamiaji (picha ya zamani).
Wiki hii Donald Trump atatoa agizo jipya kuhusu uhamiaji (picha ya zamani). REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Majaji walionyesha agizo la kwanza kuwa ni la kibaguzi na linavunja uhusiano wa wananci wa Marekani. Ikulu ya White House inahakikisha kwamba agizo hilo jipya litapasishwa na majaj.

Wakati ambapo majaji wa California walipotoa uamuzi wao, walieleza kuwa serikali haikutoa ushahidi wa tishio ambalo linadaiwa na utawala wa Trump kama lingetekelezwa na watu waliopigwa kuingia Marekani. Na kwamba nakala hiyo ilikuwa ya kibaguzi kwa wananchi wote wa Marekani.

Ikulu ya White House inaendelea kuzungumzia "usalama wa taifa" lakini haina jingine chaguo bali kuzingatia uamuzi wa mahakama. "Tunaadaa agizo jipya, kwa kufikia lengo hilo, kwa kuheshimu kile mahakama ilichosema, mpaka tutakaposhinda , alisema Sean Spicer.

Sean Spicer anaendelea kuwa na matumaini ya kushinda katika mahakama dhidi ya Jimbo la Washington lakini anakiri kwamba ni lille lile la kulinda usalama wa taifa la Marekani.

Rais Trump kuongeza vigezo, kukabiliana na wahamiaji

Hayo yakijiri Wizara ya usalama wa ndani ya nchi, nchini Marekani, ina mipango ya kuwaajiri maelfu ya maafisa wa ziada, watakaohusika kutekeleza hatua kali zilizowekwa na utawala wa Donald Trump, kukabiliana na wahamiaji haramu. Maelekezo hayo yametolewa baada ya utawala wa Trump kusema kuwa, wahamiaji wasio na stakabadhi maalum ya kuishi Marekani na walio na rekodi ya uhalifu, wanahatarisha maisha ya wananchi wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.