Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-USAFIRI

Trump kutangaza mikakati mipya ya kiusalama

Baada ya Mahakama kuu nchini Marekani kutupilia mbali rufaa ya rais Donald Trump, aliyetaka kuondolewa kwa zuio la awali la kuingia nchini humo kwa wageni na wakimbizi kutoka mataifa saba, Jumatatu hii anatarajiwa kutangaza mikakati mipya ya kiusalama inayoendana na amri yake ya awali.

Rais wa Marekani Donald Trump atangazia kutangaza mikakati mipya ya kiusalana
Rais wa Marekani Donald Trump atangazia kutangaza mikakati mipya ya kiusalana REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mwishoni mwa juma, rais Trump, amesema mahakama zimegeuka kuwa za kisiasa na kupinga amri za rais ambazo ni wazi zina lengo la kulinda usalama wa taifa hilo dhidi ya watu wasio waaminifu.

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuzungumza kwa simu na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na mwenzake wa Nigeria Muhamadu Buhari.

Hata hivyo, raia wa Nigeria watakuwa wanasubiri kusikia walichozungumza viongozi hawa kwa sababu rais wao amekuwa nchini Uingereza akipata matibabu, bila ya taarifa zozote rasmi kuhusu maendeleo yake.

Hii ndio itakuwa mara ya wa kwanza kwa mazungumzo rasmi kati ya rais Trump na viongozi wa Afrika tangu kuapishwa kwake mwezi uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.