Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-VISA

Utawala wa Trump kukata rufaa dhidi ya kizuizi cha agizo la Uhamiaji

Jumamosi Februari 4 Wizara ya sheria ya Marekani imeonyesha nia yake ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa jaji wa Seattle ambaye alisimamisha amri ya Donald Trump inayopiga marufuku raia kutoka nchi saba za Kiislamu kuingia nchini marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa West Palm Beach, Florida, Februari 3, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa West Palm Beach, Florida, Februari 3, 2017. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani amemshambulia kwa maneno makali Jaji James Robart, na kuahidi kwamba uamuzi wa "ujinga" wa 'mtu anayejidai kuwa ni jaji" utafutwa.

Jaji James Robart alisimamisha kwa muda utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia kutoka mataifa saba ya Kiislamu kuingia nchini Marekani.

Jaji wa Seattle alipuuzilia mbali sababu zilizotolewa na mawakili wa Serikali na kusema kuwa amri hiyo inaweza kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa mahakamani.
Serikali imesemai itakata rufaa ya dharura dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, ambao ni changa moto kubwa kwa utawala wa Trump.

Serikali ya Marekani inasema kuwa makumi ya maelfu ya visa zimefutiliwa mbali tangu rais Trump kutia sahihi amri ya kupunguza idadi ya watu wanaopaswa kuingia nchini Marekani juma lililopita.

Katika hotuba yake ya kila juma, rais alisema amri yake ilikusudiwa kuwalinda Wamarekani.

Wakati huo huo Idara ya forodha ya Marekani imeyaambia mashirika ya ndege kwamba waruhusu abiria kupanda ndege kuelekea Marekani abiria ambao walinyimwa ruhusa baada ya Rais Trump kutoa amri kwamba watu kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi, wakataliwe kuingia Marekani.

Shirika la ndege la Ghuba, Qatar Airways, lilisema litaanza kupakia abiria haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.