Pata taarifa kuu
BRAZIL-USALAMA-HAKI

Mauaji mapya yatokea katika gereza la Natal

Nchini Brazil, watu wasiopungua kumi wamepoteza maisha baada ya makabiliano mapya kati ya makundi mawili ya wahalifu wanaozuiliwa jela. Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, Januari 15 katika jela la Alcaçuz katika mji wa Natal, kaskazini mwa nchi.

Makundi hasimu ya wafungwa juu ya paa la gereza la Alcaçuz, Januari 14, 2017.
Makundi hasimu ya wafungwa juu ya paa la gereza la Alcaçuz, Januari 14, 2017. HO / TV PONTA NEGRA SBT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vitengo maalum vya polisi na jeshi vilitumwa katika eneo la tukio ili kuingilia kati. Pamoja na vifaa muhimu, magari kadhaa ya kivita na helikopta, hatimaye vikosi vya usalam vilifaulu kuingia katika gereza hilo. Hata hivyo wafungwa walikabiliana na polisi ili isiwezi kuingia katika jela. Wafungwa hao walikua walijihami vya kutosha na kuzuia polisi kuingilia kati, pia walikata umeme.

Makabiliano hayo yalidumu masaa 13 na polisi walichukua udhibiti wa jela hilo siku ya Jumapili alasiri.

Kwa mujibu wa viongozi tawala katika jimbo la Rio Grande do Norte, mauaji hayo ni matokeo ya vita kati ya makundi mawili ya wahalifu wanaopigania udhibiti biasha ya madawa ya kulevya: "Kundi la kwanza katika mji mkuu wa Brazil linajulikana kwa jina PCC, kutoka Sao Paulo, na kundi jingine linalojiita Vermelho (CV) ambapo makao yake makuu ni Rio de Janeiro. Katika gereza la Alcaçuz, PCC lina uhasama na kundi jingine la wahalifu lenye mafungamano na kundi la Vermelho (CV).

Uhasama huu mpya ni katika mfululizo wa makabiliano mabaya yaliyotokea katika magerza matatu nchini Brazil tangu mwanzoni mwa mwaka huu na ambayo tayari yamesababisho vifo vya watu wengi.

Mashirika ya haki za binadamu mara kwa mara yanakosoa mazingira mabaya wanakozuiliwa wafungwa nchini Brazil ambapo magereza yanakumbana na vurugu zinazohusishwa na biashara ya madaw ya kulevya, msongamano na rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.