Pata taarifa kuu
MAREKANI

Police waimarisha usalama kwenye mji Charllote baada ya kuuawa na Polisi kwa kijana mweusi

Polisi mmoja amekufa na wengine zaidi ya 12 wamejeruhiwa wakati wa maandamano yaliyokuwa ya vurugu kwenye mji wa North Carolina, machafuko yaliyozuka baada ya Polisi kudaiwa kumpiga risasi hadi kufa kijana mweusi mwenye asili ya Afrika.

Police kwenye mji wa Charlotte nchini Marekani wakijaribu kuwazuia waandamanaji wanaopinga kuuawa kwa kijana mweusi na Polisi, 21 September, 2016.
Police kwenye mji wa Charlotte nchini Marekani wakijaribu kuwazuia waandamanaji wanaopinga kuuawa kwa kijana mweusi na Polisi, 21 September, 2016. REUTERS/Adam Rhew/Charlotte Magazine
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji walijikusanya usiku wa kumakia Jumatano ya September 21 jiranik na maduka makubwa mjini Charlotte ambako tukio hili lilitokea, wakiwa wamebeba mabango yanayosomeka “Black Lives Matter” wakiimba “hakuna haki! Hakuna aman!”.

Taarifa kutoka kwenye mji huo zinasema kuwa mtu aliyepigwa risasi na Polisi wa kituo cha Charlotte-Mecklenburg, ametambuliwa kwa jina la Keith Lamont Scott.

Mkuu wa kitengo cha Polisi cha Charlotte-Mecklenberg, amethibitisha kifo cha kijana huyo na kuongeza kuwa Polisi wake wanne walijeruhiwa wakati wa makabiliano na waandamanaji.

Taarifa zaidi kutoka kwenye mjik huo zinasema kuwa Polisi, Brentleu Vinson aliyehusika kwenye tukio hilo, tayari amepewa likizo yenye malipo wakati huu uchunguzi ukiendelea.

Tukio hili linajiri ikiwa imepita miezi kadhaa toka kushuhudiwa kwa maandamano kama haya nchini Marekani, kupinga vitendo vya ubaguzi vinavyidaiwa kutekelezwa na Polisi weupe dhidi ya vijana weusi.

Rais wa Marekani Barack Obama ametaka uwepo wa utulivu wakati huu tukio hili likichunguzwa na mamlaka husika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.