Pata taarifa kuu
MAREKANI-HILLARY CLINTON

Hillary Clinton kuanza kampeni yake Alhamisi

Baada ya kulazimika kupumzika kufuatia hali yake kuzorota, Hillary Clinton akiungwa mkono na Rais Barack Obama dhidi ya "upinzani usio halali" anaanza kampeni zake Alhamisi hii. Wafuasi wa chama cha Democratic walikua na wasiwasi kuhusu afya ya mgombea wao katika uchaguzi wa urais uliyopangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Mgombea urais katika chama cha Democratic yuko katika mapumziko tangu kuzorota kwa afyake Jumapili, Septemba 11, 2016.
Mgombea urais katika chama cha Democratic yuko katika mapumziko tangu kuzorota kwa afyake Jumapili, Septemba 11, 2016. REUTERS/Brian Snyder
Matangazo ya kibiashara

Hillary Clinton atakua katika jimbo la North Carolina Alhamisi hii Septemba 15 kwa mkutano wa kwanza tangu tatizo lake la afya. Mgombea amekua katika mapumziko tangu kuzorota kwa afya yake Jumapili, Septemba 11 tatizo ambalo lilizua utata juu ya afya ya wagombea wa urais. Hillary Clinton alikutwa na maradhi ya Nimonia ingawa cheti cha hivi karibuni kutoka kwa daktari wake kinasema yuko sawa kiafya kushikilia nyadhifa za juu.

Hillary Clinton amekua akikosolewa na kambi ya Republican kwa kusema kwamba nusu ya wapiga kura wa mpinzani wake Donald Trump walikuwa watu "wenye udhalili".

"Alikashifiwa na kambi ya mrengo wa kulia wakati mwingine kambi ya mrengo wa kushoto," Bw Obama amesema katika mkutano wa hadhara mjini Philadelphi. "Alituhumiwa makosa mbalimbali na alikosolewa kuliko mtu yeyote."

Zikisalia siku 13 za mjadala dhidi ya Donald Trump na ikisalia miezi miwili ya uchaguzi wa rais, Bii Clinton, mwenye umri wa miaka 68, anaendelea kupumzika katika makazi yake ya Chappaqua, kaskazini mwa mji wa New York, baada ya hali yake ya afya kuzorota Jumapili wakati wa maadhimisho ya Septemba 11.

Msemaji wake Nick Merrill alitangaza kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ataanza tena kampeni zake Alhamisi wiki hii.

Barack Obama katika mkutano wa kumuunga mkono mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton, mjini Philadelphia, Septemba 13, 2016.
Barack Obama katika mkutano wa kumuunga mkono mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton, mjini Philadelphia, Septemba 13, 2016. REUTERS/Carlos Barria

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.