Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAQ-ASHTON CARTER

Carter atangaza kupelekwa Iraq mamia ya askari wa ziada

Mkuu wa Pentagon Ashton Carter ametangaza Jumatatu hii mjini Baghdad, kutuma mamia ya askari wa ziada nchini Iraq ili kusaidia vikosi vya serikali kupambana dhidi ya wanajihadi wa kundi la Islamic State (IS) na hasa kuuteka mji wa Mosul.

Ashton Carter, kiongozi wa Pentagon.
Ashton Carter, kiongozi wa Pentagon. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika ziara yake ya nne nchini Iraq tangu kuteuliwa kwenye nafasi hiyo mwezi Februari 2015, Bw Carter amekutana na Waziri Mkuu Haider al-Abadi na mwenzake Khaled al-Obeidi, wakati ambapo Marekani inaongoza muungano mpana wa kimataifa unaopambana dhidi ya kundi la IS.

Ziara yake inakuja siku mbili baada ya vikosi vya Iraq kuiweka chini ya himaya yao kambi ya Qayyarah, kilomita 60 kusini mwa jimbo la Mosul, ikionekana kama hatua muhimu katika vita vya kuuteka mji wa pili wa Iraq unaokaliwa na kundi la Islamic State (IS) tangu mwezi Juni 2014.

"Kutokana na kusonga mbele hivi karibuni kwa vikosi vya usalama, Bw Carter ametangaza kuwa Marekani, katika uratibu wa karibu na Serikali ya Iraq itatuma askari 560 wa nyongeza nchini Iraq ili kuendelea kupambana dhidi ya kundi hili la kigaidi," imebaini taarifa kutoka Pentagon.

"Idadi hii ya ziada itatoa msaada kwa vikosi vya Iraq hasa katika suala la uwezo wa vifaa na miundombinu katika kambi ya Qayyarah," Bw Carter amesema.

Idadi hii ya askari wa ziada itapelekea idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Iraq kuongezeka na kufikia askari 4,600, hasa kwa ajili ya ujumbe wa mafunzo kwa askari wa Iraq.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.