Pata taarifa kuu
ECUADOR-TETEMEKO

Idadi ya watu waliopoteza maisha Ecuador imefikia 413

Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lilipiga pwani ya Pasifiki ya Ecuador Jumamosi Aprili 16 imeongezeka na kufikia 413 na watu zaidi ya 2,600 ndio wanasadikiwa kuwa wamejeruhiwa.

Idadi ya vifo kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Ecuador imeongezeka Jumatatu hii, Aprili 18, 2016.
Idadi ya vifo kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Ecuador imeongezeka Jumatatu hii, Aprili 18, 2016. REUTERS/Guillermo Granja
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa Idara za huduma za dharura wameendelea na shughuli ya uokozi kujaribu kuwaondoa watu ambao bado hai waliofunikwa chni ya vifusi. Maafisa hao wanasaidiwa na timu nyingine kutoka nchini zingine. Rais Rafael Correa alitembelea Jumatatu maeneo yaliyoathirika.

Watu watano waliokolewa Jumatatu hii asubuhi katika mji wa Manta. Walikua walinaswa chni ya vifusi vya jengo la biashara. Kaskazini mwa nchi hiyo, katika mji wa Pedernales, msichana mmoja ndio alionusurika baada ya kufanya masaa 20 chini ya vifusi vya nyumba.

Kwa upande wake Rais Rafael Correa, ambaye alitembelea mji huu ulio karibu na kitovu cha tetemeko lililopiga nchini humo Jumamosi, ametangaza hali ya dharura. "Kipaumbele chetu ni usalama. Tunapaswa kuokoa maisha ya watu wengikadri tuwezakanavyo, kuwaletea maji, chakula na kuhakikisha usalama wao. Baadaye tutalazimika kuijenga upya Pedernales, mji wa Portoviejo, wilaya ya Manta katika jimbo la Tarqui, miji ya Jama na Canoa. Itachukua miezi na miaka na pengine gharama ya mabilioni ya dola, "alisema jana Jumatatu Rais wa Ecuador Rafael Correa.

Hali ya dharura imetangazwa katika majimbo sita, yenye watu milioni 16.

Mitandao ya kijamii ili kupata watu waliotoweka

Wakati huo huo, sehemu nyingi za nchi bado zimetengwa kutokana na kuharibika kwa miundo mbinu. Helikopta zimetumwa ili kuwasafirisha watu waliojeruhiwa, lakini msaada haujawasili, barabara zimeharibika na ni vigumu kutembelea maeneo hayo.

wakazi wengi wa maeneo hayo wamekua wakitumia mitandao ya kijamii kuwatafuta ndugu na jamaa zao, waliotoweka tangu tetemeko hilo kupiga katika maeneo hayo.

Rais Correa atatembelea Jumanne hii katika vijiji kadhaa ambavyo haviingiliki. Ametangaza uamuzi wake wa kubaki wiki nzima katika maeneo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.