Pata taarifa kuu
ECUADOR-TETEMEKO

Idadi ya vifo Ecuador yaendelea kuongezeka

Rais wa Ecuador Rafael Correa ameonya kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini humo huenda ikaongezeka kutoka 272.

Mji wa Pedernales, katika pwani ya Pasifiki, umekumbwa zaidi na tetemeko la Aprili 16, 2016.
Mji wa Pedernales, katika pwani ya Pasifiki, umekumbwa zaidi na tetemeko la Aprili 16, 2016. RODRIGO BUENDIA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inakuja kipindi hiki wasiwasi kuendelea kushuhudia kuhusu hatima ya mamia ya watu ambao hawajapatikana hadi sasa.

Hata hivyo, rais Korea amezipa moyo familia ambazo wapendwa wao hawajapatikana na kuwaambia kuwa uchunguzi umebaini kuwa kuna watu ambao bado ni wazima lakini wamefunikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

Watu wengine zaidi ya elfu mbili walijeruhiwa baada ya kutokea kwa tetemeko hio baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Hali ya hatari imetangazwa nchini humo na wanajeshi zaidi ya 10,000 na polisi zaidi ya elfu tatu wanasaidia katika juhudi za kuwatafuta watu ambao hawajapatikana hadi sasa hivi.

Tetemeko hilo limesabisha nchi jirani ya Peru kutangaza uwezekano wa kutokea kwa Tsunami katika nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.